WANACHI WA MPWAPWA WAMTAKA WAZIRI LUKUVI KUWAANZISHIA BARAZA LA ARDHI LA WILAYA.
Na Steph noel Mpwapwa
WANANCHI
wa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wamemuomba waziri mwenye dhamana ya Wizara ya Ardhi Nyumba na makazi Mhe , Wiliam Lukuvi kuwaanzishia
Baraza la Ardhi la wilaya kufuati usumbufu wano upata kufuata huduma
hizo katika wilaya ya Dodoma mjini.
Walisema huwalazimu kusafiri umbali wa zaidi
ya kilomita 90 hadi 110 kutafuta huduma
za kishria juu ya migogoro ya ardhi na
mipaka.
Wanachi hao yaliyasema hayo kwa nyakati
tofauti wilayani hapa walipokuwa wakiongea na Majira juu ya usubufu wanao upata kufutia kutafuta
haki zao za migogoro ya ardhi iliyo shindikana ngazi ya mabaraza ya kata na hivyo huwalazimu kutumia muda mrefu na
gharama nyingi, na wengine wakiacha kufuatilia haki zao hizo kutokana na
kushidwa gharama .
Mmoja wa wakazi wa wilayani hapa bwana Alex Mwarabu mkazi wa kijiji cha Kisokwe alisema kumekuwako na usumbufu mkubwa
unaotokana na huduma nyingi za kutafuta
haki kuwa mbali na hivyo hupelekea baadhi ya watu kukosa haki zao za msingi
hasa za migogoro ya mashamba kutokana mabaraza ya aridhi ya wilaya kutokuwapo katika ngazi za chini hasa mawilayani.
Aidha Mwarabu alisema kuwa kufutia hali hiyo inachangia kuchochea mogogoro ya ardhi lakini pia kuongeza uhasama hadi vifo
maeneo ya vijijini ambapo ndiko migogoro mingi ya ardhi inazidi kushika kasi
hasa katika kipindi hiki.
Aliongeza kuwa “haiwezekani mtu anaona ana haki yake na inaporwa na wenye
nacho na sehemu za kukatia rufaa iko mbali
na hana uwezo ndo maana huamua kuchukua njia mbadala ambayo huweza kusababisha vifo, au uhasama katika jamii”alisema Mwarabu
Mwarabu pia aliziomba mamlaka husika ngazi ya halmsahauri kuweza
kuzungukia na kuona utendaji wa mabaraza
ya ardhi ya kata kwa kile alicho kisema
kuwa baadhi ya wajumbe wa mabaraza hayo kuyageuza na kuwa sehemu za
kutafutia pesa kwa kuwanyonga haki zao
watu wanyonge wasio kuwa na pesa ndio hunyimwa haki.
Tena alitaka serikali ibadilishe mfumo wa
mabaraza kata ambayo kwa sasa
hujiendesha kwa kujitolea kitu alicho kisema kinachochea mianya ya rushwa na kusababisha malalamiko mengi kwa wananchi
wenye kipato cha chini.
Mwanasheria
wa halmashauri ya wilaya ya mpwapwa na Wakili Bi Dorica Doria alikili halmashauri
kuto kuwa baraza la Ardhi la wilaya
, kitu alicho sema kuwa kinaongeza
usumbufu mkubwa kwa wakazi wa
mpwapwa na kata zake 33.
Hata hivyo Bi Dorica alisema
kuwa jukumu la kuanzisha mabaraza
hayo yako chini ya Waziri mwenye dhamana
ambae ni waziri wa ardhi nyumba na makazi .
“Sheria ya mabaraza ya Ardhi na nyumba ya
mwaka 2002 kifungu cha 22 kifungu cha sheria hiyo namba 167 na 168 ya sheria ya vijiji namba 14
ya mwaka 1999 inampa waziri mwenye dhamana kuweza kuanzisha hayo kwa kila wilaya ,
Kanda na Mkoa”aliongea Bi Dorica
Lakini alisema kuwa serikali inashidwa
kufanya hivyo kutokana na ukosefu wa fedha za kuendeshea mabaraza hayo
ambayo katika kila wilaya hapa nchini.
Comments
Post a Comment