MVUA ZASABABISHA MAFURIKO GULWE MPWAPWA
Na Stephen noel
–Mpwapwa.
Zaidi ya kaya 30 za
kijiji cha Gulwe wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma hazina mahala pa kuishi
kufutia mvua kubwa ilionyesha usiku wa
kuamkia jana na kusababisha nyumba zao kubomoka katika kijiji hicho.
Sambamba na nyumba hizo
kubomoka pia mvua hiyo imeharibu hekali 47 zamashamaba ya mazao mabli mbali yalisomwa na maji .
Diwani wa kata ya
gulwe bwana Gabriel Kizige alisema
pamoja na maafa hayo pia yamesabaisha
zaidi ya kaya 50 nyumba zao kuingiliwa na kusababisha badhii ya mali kuharibika
ikiwemo chakula na mali zingine .
Akitotaarifa ya madhara
yaliyo patikana mbele ya kamati ya maafa
mwenyekiti wa kijiji cha gulwe Bwana Peter Sogodi alisema kuwa nyumba 30 za
wakazi wa gulwe zilimomoka na nyumba 50 zilingia maji na hekali 47 za
mazao mbalimbali ziliharibika kwa
kusobwa na maji.
Aidha ofisa mkaguzi
wa njia ya treni Steshen Gulwe bwana
Moses Magoha alisema pia mvua hiyo imesababisha hasara katika njia ya reli
hiyo kwa kufukiwa kwa mchanaga , na zaidi mita 26 za reli imeobolewa
na na mvua hiyo.
Akiongea mmoja wa
wananchi wa kjiji hicho bi Elizabeth
Stephen alisema kuwa mvua hiyo ilinza kunyesha majira ya saa tisa alfajili na kusababisha maafa hayo katika kijiji chao
ambapo pamoja na kuwa kaya nyingi
zilikuwa zinakabiliwa na njaa pia
mafuriko hayo yameongezea kwakusoma chakula chote kilicho kuwepo cha kuweza
kujikimu.
Hata hivyo bwana Bakari Mlisho
alisema kuwa kaya zilizo adhilika
na mafuriko hayo ni zile ambazo baada ya kuhamishwa na uongozi wa wilaya ya mpwapwa walirudi tena katika makazi
yao ya zamani ambayo sehemu hiyo ni ya
mkondo wa maji na sehemu hatarishi kwa makazi.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa kamati ya maafa ya wilaya ya mpwapwa ambae ni mkuu wa wilaya
hiyo bwana Mohamed Utaly amewataka waaadhilika wa
mafuriko hayo kuto kurudi tena katika makazi hayo ya zamani ambayo ni hatarishi kwa maisha yao.
Aidha alisema kwa hatua
za awali wanachi hao waweze kusaidiana katika uwezo walio kuwa nao,pia serikali
itatumia sehemu ya chakula cha njaa kuweza kusaidia kaya zilizo adhirika na
mafuriko kwa sehemu kubwa.
Comments
Post a Comment