MKURUGENZI MTENDAJI MPWAPWA AWATAKA WATENDAJI WAKE KUACHA URASIMU.
Na Stephen noel
–Mpwapwa
MKURUGENZI mtendaji wa halmashauri ya wilayaya mpwapwa
mkoani Dodoma Bwana Mohamed Maje amesema kuwa atahakikisha anakomesha urasimu wote kwa watendaji wake wa
chini kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza wilayani hapa.
Mkurgenzi huyo ameyasema
hayo wilayani hapa walipotembelea kiwanda kidogo cha kusindika siagi ya
karanga kilichopo mjini hapa mtaa wa mji
mpya.
Maje amesema
hatavumilia kuona watendaji wake wa chini wanawakwamisha wawekezaji wanao taka
kuwekeza mpwapwa.
Meneja wa kiwanda cha
kusindika karanga wilaya hapa bi Paulina Visent amesema kuwa
wamekuwa wakipata shida kutoka idara
ya ardhi kupata eneo maluumu la kujenga kiwanda hicho kwa kile alicho kisema kuwa kinakwamisha na kurudisha nyuma moyo wawekezaji wengine
wanao taka kuwekeza katika wilaya ya
mpwapwa kutokana na urasimu wanao upata kutoka kwa watendaji wa serikali.
Aidha amesema kiwanda
hicho kimesaidia kuitangaza Mpwapwa katika nyaja za kibiashara kwa mikoa ya
jirani na nje Tanzania kutokana na bidhaa inayotengenezwa katika kiwanda chake .
Aidha Bi Paulina amesema
kuwa pamoja na mpwapwa kutangazwa pia imeweza kuajili zaidi ya akina
mama na vijana 20 ambao wanajipatia
kipato na kuinua maisha yao kutokana na kuwapo kwa kiwanda hicho
mjini mpwapwa.
Bi Paulina ameiiomba
serikali kuweza kuwasaidia kuwatafutia masoko
ya uhakika ya bidhaa wanayo
zalisha katika kiwanda chao tofauti na sasa ambapo soko lao si la uhakika sana na kusabaisha
uzalishaji kuwa mdogo.
Kwa upande wake mkuu wa
wialaya ya Mpwapwa Mohamed Utaly amewataka wawekezaji wote wanao ingia mpwapwa
kuweza kufuata taratibu zote za kisheria ili kuweza kufanya kazi kwa uhuru na kuongeza ufanisi wa kiwanda chao.
Hata hivyo mkuu wa wilaya huyo amesema kuwa atahakikisha wialaya yake inaandaa mazingira wezeshi na
yasiyo kuwa na vikwazo kwa
wawekezaji wanaoataka kuwekeza
katika wilaya ya Mpwapwa ili kuweza
kuinua kipato cha wilaya na mkoa kwa ujumla
Comments
Post a Comment