MPWAPWA YAMLIZA KAPONDA KIELIMU
OFISA elimu mkoa wa
Dodoma Bwana Juma Kaponda (JJ)amewataka
wataalamu ,wanasiasa, na walimu kushirikiana
katika kushughulikia changamoto
za Elimu ili kuweza kuinua elimu
wilayani hapa.
Kaponda aliyasema
hayo wilayani hapa katika mkutano wa wadau wa elimu uliojumuisha , walimu wakuu wa shule zote,
waratibuelimu kata , na na maofisa wa
elimu , uliofanyika katika ukumbi wa
chuo cha ualimu Mpwapwa juu ya
kutadhimini matokeo ya darasa la
saba ya mwaka 2015.
Kaponda alisema
katika mtihani wa kumaliza elimu
mwaka 2015 wilaya ya mpwapwa ilikuwa
wilaya ya mwisho kimkoa na ilikuwa wilaya ya 164 kati wilaya 166 nchi
zima ,japo ilifanikiwa kutoa mwanafunzi wa kwanza kimkoa kutoka katika
shule ya Mazoezi Mteajeta mwanafunzi
Airene Chiwanga
Aidha alisema ufundishaji
mbovu,utendaji wa kimazoea kwa
maofisa Elimu , kukosekana kwa mawasiliano sahihi kati walimu na maofisa
elimu imepelekea Mpwapwa kushidwa kufanya vizuri katika mtihani huo kwa mika miwili mfululizo.
Pia alisema mwamko
mdogo wa elimu katika wilaya ya Mpwapwa
imepelekea elimu kuzidi kudidimia siku hadi siku kitu alicho kisema kuwa kimesababishwa na na ulegevu wa usimamizi wa sheria kwa viongozi wa ngazi za vjijiji na kata.
Alisema”kwa mfano kwa
watoto walioanza darasa la kwanza mwaka 2010 walikuwa watoto 8048 lakini kufika darasa la sita mwaka 2015
zaidi ya watoto 1702 walikuwa hawapo shueni sawa na asilimia 21% ya wanafunzi
wote walioacha masomo kwa sababu mbalimbali”alisema Juma kaponda.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mwalimu Mohamed Utaly aliyekuwa
mgeni rasmi katika mkutano huo aliwataka
viongozi wote wanao husika na suala
la elimu kuiondoa Mpwapwa katika nafasi ya mwisho kimkoa
nakuipandaisha hadi nafasi ya
kwanza kama ilivyokuwa ikifanya miaka ya nyuma.
Alisema
“sitakubali kuona Mpwapwa
ikiendelea kuto kufanya vizuri katika suala la elimu ukizingatia Mpwapwa inaongozwa na walimu nikiwamo mimi
mwenyewe na mkurugenzi wangu sasa
tujipange tuu kabla hatujanza kutumbuana
majipu”alisema Utaly.
Hata hivyo
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya
ya mpwapwa Mohamed Maje alisema
watahakikisha wanaipandisha elimu
katika wilaya ya mpwapwa kwa
kuindoa changamoto zote zilizo
kuwapo awali ikiwamo kulipa madeni ya
walimu na upandaji wa madaraja kwa
walimu wanao stahili.
Maje alisema
kuwa shule kumi za mwisho aliwataka walimu na waratibu elimu kata
kutoa maelezo ya maandishi ndani ya siku saba juu ya sababu zilizo pelekea shule
hizo kufanya vibaya.
Mmoja wa Walimu mjini
hapa Mwalimu Mohamed Matula alisema
mazingira magumu ya walimu wilayani hapa yanayo sababishwa na Jiografia
ya wilaya kunapelekea mpwapwa kuendelea
kufanya vibaya katika sula la elimu , na
mgowanyo mbovu wa walimu pia imekuwa chanzo cha
baadhi ya shule kuendelea kufanya vibaya.
Akizitaja shule kumi zilizofanya vibaya
wilayani hapa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mpwapwa bwana
Majealisema ni Shule ya Msingi Gomuhungile,Idodoma,Kazania ,Chang’ombe ,Rufu,
na Kiboriani,shule zingine ni shule ya msingi Kilambo, Njiapanda , Ngalamilo ,Mlunduzi, na
Vikundi.
Na shule zilizofanya
vizuri ni shule ya msingi
Kikombo,Pwaga,Mtejeta,Mpwapwa, Mang’angu, na Makutupa, shule zingine ni
Kimagai, Chazungwa, Lumuma, na Bumira.
Comments
Post a Comment