SERIKALI YAKANUSHA WANANCHI KUPIKA MAWE MPWAPWA



Na Stephen noel – mpwapwa
SERIKALI wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma  imekanusha taarifa za watu wa wilayani hapo kuchemsha mawe  kwa ajili ya kukosa chakula kutokana na kukikdhili kwa njaa.
Kauli hiyo  imetolewa na mwenyekiti wa kamati ya maafa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mwl,Mohamed Utaly alipokuwa ikitoa taarifa ya hali ya njaa kwa mkurugenzi wa idara ya uratibu wa maafa  kutoka ofisi ya waziri mkuu  Brigedia  Jenerali  Mbazi Msuya.
Mwl.Utaly  amesema kuna vyombo vya  habari na mitandao ya kijamii imeripoti kuwa  wananchi wa  wilaya ya mpwapwa hulazimika  kupika mawe  na pumba kwa ajili ya kujikimu   na njaa kutokana na wilaya  hiyo kukubwa na njaa kwa hali ya juu.
Aidha Mwl.Utaly amekili  kuwepo kwa hali ya njaa katika  wilaya hiyo  lakini alisema haiko kwa kiasi ambacho kimelipotiwa katika vyombo vya habari hadi wananchi kupika mawe na  pumba .
Mmoja wa  wa wananchi wa kijiji cha Chunyu  bwana Edward Kusena ambae ni mkulima mkuubwa wa zao la mhogo kijiji hapo amesema  njaa katika kijiji hicho na wilaya nzima imesababishwa na baadhi wananchi kuupuzia maagizo ya wataalamu ya kulima mazao yanayo stahimili ukame na yanayo komaa haraka  kama mhogo,matama na uwele kwa wilaya zenye mvua kidogo kama Mpwapwa.
Afisa kilimo,  uvuvi na umwagiliaji wa wilaya ya Mpwapwa Bi Justina Munisi  alisema pamoja na kuwapo kwanjaa tayari kitengo cha maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu imetoa mahindi tani 200 ambayo tayari yamesha gawiwa kwa vijiji 36 kati ya vijiji68 vilivyo athiliwa na njaa kwa kiasi kikubwa.
Bi Munis alisema  njaa hiyo imesababishwa na  na ukosefu  wa mvua kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2014/2015,na wananchi kuto kufuata mazao yanayo stahili kupadwa katika kanda za mikoa ya ukame kama Dodoma na wilaya zake.
Kwa upande wake  mkurugenzi  wa idara ya maafa ofisi ya waziri mkuu  brigedia Jenaerali Mbazi Msuya aliwataka viogozi w halmashauri hiyo kuacha kuomba chakula cha msaada bali aiwataka kuomba chakula cha  njaa na mbegu ili kuweza kondokana na kuomba chakula cha njaa kila mwaka.
Pia alisema kitengo chake kitaanza kugawa mbegu  za mhogo  bure kwa wakulima watakao jiandikisha na kutaka kupanda zao hilo ambalo litaweza kuwa  mwaraobaini wa   wilaya hiyo kukubwa na njaa kila mwaka .


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.