WAZAZI WASHAURIWA KUWAKEZEA WATOTO.
Wito umetolewa kwa wazazi wote nchini kujenga moyo wa kuwawekekea watoto wao akiba mbali mbali za kimaisha ili wasipate taabu wanapo ingia utu uzima
Wito huo umetolewa na Meneja wa Bank ya NMB tawi la Mpwapwa BWANA HERMAN MASUKI hivi karibuni alipo kuwa akizindua mpango wa Ankaunt maalum kwa watoto walio chini ya miaka kumi na nane ajulikayo kama Finacial Fitness .
Bwana masuki alidai kuwa Wazazi wengi nchini hawana tabia ya kuwawekea akiba watoto walio chini ya miaka kumi na nane kitu alicho kisema kuwa kina leta shida pindi mtoto aingiapo utu uzima na kuanza au anapo pelekwa shule kushidwa kugalamiwa masomo kutokana na wazazi wengi kuto kuwa na malengo ya badae kwa watoto wao
Mhasibu wa BENK ya NMB Mpwapwa akitoa zawadi kwa wanafunzi walio hudhuria harmbee ya fitness M pwapwa (picha na noel Stephen mpwapwa.
Bwana Musuki alidai kuwa wazazi waweze kuwa fungula watoto wao akaunti ijulikanyo kama junior account amabayo alisema kuwa ni ankunti iliyo wekwa mahususi kufundisha watoto njisi ya kuweka fedha kwa ajili ya matumizi ya baadae.
Alisema kuwa wazazi wakumbuke kuwa “iku zote maandalizi ya kesho yaanaanza leo kwahiyo naombeni wazazi nanyi watoto kuweza kujenga tabia za kujiwekea akiba ili kuweza kuondoka na hali ya kujuta baadae”.
Aidha alisema kuwa watoto wengi wamejikuta wanaingia kwenye shida au matatizo kutokana kuto kuwa na akiba ya kuanzia maisha au kjiendeleza kibiashara na masomo.
Pia “tukumbukle kuwa sisi hatuna mkataba na mungu je watoto wangapi ambao tunawaona wazazi wao walikuwa na uwezo mkubwa wa kifedha lakini mala baada ya kufa wazazi wao tunawaona watoto wanapolwa mali na ndugu wa marehemu na kubaki hawana kitu na kuwa watoto wa mitaani je wangewekewa akiba benki nani angewadhurumu hivyo ndugu zangu tupende kujijengea tabia ya kuwawekea watoto akiba za maisha”aliongea bwana Masuki
ALISEMA kuwa Benki hiyo imeamua kuanzisha mpango huo kufuatia tafiti mbalibali zilizo fanywa na maafisa ya benki hiyo na kugundua kuwa watoto wengi wanapata shida za kumudu gharama za maisha na masomo kutokana na wazazi wengi kuto kuwa tabia za kuwawekea watoto wao akiba ya baadae.
Katika uzinduzi huo jumla ya watoto 327 walihudhuria harambee hiyo kutoka shule mbalimbali za wilya ya mpwapwa ambazo ni shule ya msingi Chazugwa,Ilolo, Mazae, Mpwapwa na Kikombo na kati hao ni watoto wacache tu walikuwa na akaunti za benki za watoto.
Comments
Post a Comment