WANAKIJIJI WAMKATAA MWEKEZAJI WA MADINI LUFUSI
NA noel Stephen mpwapwa.
MKUU wa wilaya ya Mpwapwa Bwana CHRISTOPHER KANGOYE amesitisha uchimbaji wa madini aina ya copa katika kata ya lumuma kijiji cha LUFUSI kwa kampuni ya KIMANI MINERALS LIMETED kufuatia kuto fuata taratibu na uharibifu wa mazingira .
MKUU huyo amefikia hatua hiyo kufuatia mgogoro ulioibuka kati ya mwekezaji huyo na wanakijiji wa kijiji hicho kwa madai kuwa mwekezaji huyo hajafuata taratibu za uchimbaji wa madini na kuchimba madini hayo karibu na vyanzo vya maji vya kata nzima ya lumuma na vijijiji vyake.
AKIONGEA na waandishi wa habari ofisini kwake bwana KANGOYE alikili kuwepo kwa mgogoro kati ya mwekezaji wa huyo na wanakijiji wa kijiji cha lufusi kwa madai kuwa amechimba madini hayo karibu na chanzo cha maji cha kijiji hicho na ambacho ni tegemeo la upatikaji wa maji wa kata ya lumuma na vitongoji vyake.
AIDHA KUU huyo alisema kuwa kampuni yenye leseni ya wachimabaji wadogo lakini wanatumaia mitamabo ya kisasa katika kufanya utafiti wao maboa kwao umejikita katika kuitafuta faida na kuwadhoofisha wazawa na mali zao za asili” nasema lazima tuangalie faida ya wengi na sio kuangalia faida za wachache kwa sababu siku hizi watu hao wanataka faida yao tu na si watu wengi na lazima tutunze mazingira ili yaweze kutusaidia badae.
Pia B wana Kangoye aliwa taka watu wote wanao ishi kwenye vyanzo ya maji vya kijji hicho lazima waondoke wenyewe kabala hajatumia nguvu za dola kwa ajili ya msatakabali wa wilaya ya mpwapwa na vitongoji vyake “ nasema hakuna aliye juu ya sheria hivyo wito wangu kwa wananchi na wawekezaji wafute sheria na taratibu ili kuiendeleza mpwapwa”
Alivitaja vijiji ambavyo wakazi wake wanaendesha shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji alisema kuwa ni kijiji cha Lufusi kata ya lumuma, kiboriani mpwapwa mjini na kwamdyanga kata ya mpwapwa mjini nakuwataka wahame maeneo hayo kabla hajatumia nguvu za dora.
KWA UPANDE wake meneja wa maradi wa shirika la kuhifadhi misitu ya Asili ya Tanzania Bwana LAURENT MWAKAKONYOLE alidai kuwa wawekezaji hao wameingia kwenye msitu wa asili ya kata ya lumuma na kuharibu misitu na wamechimba barabara yenye urefu wa km 8 katikati ya msitu bila kuhusisha uongozi wa kijiji amabapo alisema ni ukiukaji kwa kanuni na taratibu za nchi.
Mwakakonyole alisema shirika lao limejikita katika kuhifadhi misitu ya asili ya safu za milima ya Lubeho ambako zimeonyesha mafanikio makubwa ya kumbamabana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini na kutunza uoto wa asili katika milima ya LUFUSI kata ya lumuma .
Mtendaji wa kata kijiji hicho BWANA Jonas MBOGO aliwataka wananchi wa kijiji hicho kufuata sheria na taratibu ili kuweza kutunza mali asili zao kwa kushirikiana na wadau wanaojitokeza katika kijiji chao kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
ALISEMA kijiji chake kimejikuta kimeingia kwenye mgogoro na mchimbaji wa madini hayo kwa kukiuka sheria ya madini ya mwaka 2010 namba 95kifungu kidogo cha (1)(a) na (iv)kifungu kidogo cha pili (II) na cha (V)(c)na (e).
Comments
Post a Comment