MWANASHERIA WASERIKALI WAPINGANA NA DPP
Na noel stephen mpwapwa
TASISI ya kuzuia na kupambana na RushwaTAKUKURU wilaya ya mpwapwa Mkoani Dodoma imemfikisha mahakamani mtumishi wa halimashauri ya mpwapwa bwana Ignace Saye kwa tuhuma za ubadhilifu wa mali za umma
.
Ikisomewa mashtaka yake mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya bwana JEMSI KAREIMAHA na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU bwana GARRY NOMA alidai kuwa mtuhumiwa huyo anakabiliwa na makaosa 10 ya ubadhilifu wa mali za umma.
Bwana Garry Noma alidai mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alilitenda makosa hayo katika tarehe mbalimbali za mwaka 2008 hadi mwaka 2010 katika ofisi ya halmashauri ya wilaya ya mpwapwa akiwa kama boharia mkuu wa wilaya hiyo.
Na mtuhumiwa alikanusha makosa yote hayo na ameachiwa huru kwa dhamana ya shiliongi million 10 au kitu chenye dhani ya hiyo pesa kisichi weza kuhamishika na shitaka lake litasomwa tena 12/07/2012 .
AIDHA katika hali isiyo ya kawaida mwanasheria mkuu wa serikali kanda ya kati wametofautina kimaamuuzi na mkurugenzi mkuu wa mashitaka DPP juu ya tuhuma za kesi inayo mkabili boharia ya halmashauri ya wilaya ya mpwapwa Bwana IGNACE SAYE kwa mwanasheria kudai hana hatia wakati mkurugenzi wa mashitaka anadai Bwana Saye ana kesi ya kujibu.
PIA kwa mujibu wa chanzo chetu kimedai kuwa mwanasheria mkuu mfawidhi wa serikali kanda ya kati bwana FARAJA NCHIMBI alimwandikia barua bwana SAYE ya tarehe 20.03.2012 yenye kumb na SAD/C/120/5/2/17/2011/08 na nyingine yenye kumb na DOMR/CID/B1/7/VOLXXII/188 ya tarehe 23/03/2012 kuwa amechunguza na kuona kuwa hana hatia na hana kesi ya kujibu kutokana na kukosa nakala halisi za vielelezo vya ushahidi wa ununuzi wa mafuta katika ya kuendeshea mitambo ya kutengeza daraja la GODEGODE ambapo pia nakala moja ikienda kwa mkurugrenzi wa mashataka DPP. Kwa taarifa.
KWA UPANDA WAKE mwendesha mashtaka ya Tasisi ya Kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU bwana NOMA alidai kuwa mtuhumiwa anashitakiwa kwa mujibu ya sheria ya kuzuia na kupambana na no 11 ya mwaka 2007 anashitakiwa kwa kuhujumu uchumi aya 1jedwali 10 kifungu 57(1) na kifungu cha 60(2) sura na 200R:E2002.
Bwana SAYE anaye kabiliwa na tuhuma za ubadhilifu wamali za umma na na kosa la kumdanganya mwajili wake kwa kugushi na nyaraka za kununulia mafuta za kuendeshea mitambo yenye dhamani ya shilingi milioni 12,150,400/
PIA kwa upande wake mtuhumiwa bwana saye ametoa lawama kwa utendaji wa serikali na tasisi zake kuwa hazina mawasiliano mazuri na juu uendeshaji wa kesi zinazo ikabili serikali “kwa maana mwanasheria kasema mimi sina hatia pccb wananipeleka mahakamanin kwa kosa hilo hilo sasa nashidwa kuelewa labda kuna kingine wanacho kitaka kwangu maana pccb wantumia sheri gani na polisi na wanasheria wanatumi sheria zipi mbona wanachanaganyana wenyewe”, alisisitiza bwana saye.
Bwana Saye na wanzake watatu walituhumiwa kugushi nyaraka za kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo ya ujenzi wa daraja la godegode liligharimu kiasi cha sh million 950 ambalo lilijengwa na wanajeshi kuanzia mwaka 2008 nhadi 2011, na alisimamishwa kazi kwa uchunguzi wa kesi hiyo na walipotambua hana hati amerudishwa tena kazini na tena bado anakabiliwa na shitaka hilohilo.
Comments
Post a Comment