Posts

DC MPWAPWA AHIMIZA TEKNOLIJIA ITUMIKE KUPUNGUZA MALARIA NCHINI.

Image
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Mpwapwa.   Mkuu  wa wilaya ya Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma, Mh. Jabir Shekimweri, amewaagiza wataalamu wa mifumo ya teknolojia hapa nchini kuang alia uwezekano wa kuitumia mifumo hiyo kwa kutoa elimu ya namna ya kudhibiti malaria hasa katika maeneo ya vijijini. Mh. Shekimweri ameyasema hayo wilayani Mpwapwa alikupowa akizindua mpango wa matumizi salama ya vyandarua vyenye dawa vilivyotolewa na Serikali kwa lengo la kutokomeza malaria hapa nchini mafunzo yaliyofanyika mjini Mpwapwa. Mkuu wa wilaya hiyo  amesema kwa nyakati  hizi, simu za mikononi zenye mitandao ya kijamii zimeenea kila mahala, hivyo ikiwepo namna nzuri ya kufikusha ujumbe utakaosaidia wananchi kufanya usafi wa mazingira yanayowazunguuka, kuna uwezekano mkubwa wa kupunguza mazalia ya mbu wanaosababisha maambukizi ya Malaria. Mafunzo hayo yamewashirikisha wataalamu mbalimbaalia kutoka wilaya za Kongwa na Mpwapwa ...

WAGOMBEA WAKUMBUSHWA KUJIEPUSHA NA RUSHWA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI.

Image
. Mpwap wa .   Mkuu wa Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa wilayani Mpwapwa Bi Julieth Mtuy akiwakumbusha madiwani wa Halmashuri  ya Mpwapwa juu ya sheria ya Uchaguzi.  Mpwapwa Mkuu   wa tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani Mpwapwa   mkoani Dodoma   Bi Julieth Mtuy   amewatahadharisha   wanasiasa wanao taka kuwania   nafasi za ubunge na udiwani katika   Majimbo ya     Mpwapwa   na Kibakwe kutojihusisha   na vitendo vya rushwa wakati wa kuelekea katika chaguzi     mkuu. Mtuy ameyasema hayo na kuwakumbusha wagombea wa vyama vyote   kuto jihusisha na vitendo vyovyote vya utaoji wa rushwa kushawishi au kumchafua   mgombea mwenzie kama inavyo elekeza sheria ya gharama za uchaguzi namba 6 ya 2010 kuanzia k ifungu 15,21-23 kinachomtaka mgombea kuweka wazi ghalama za uchaguzi   atakazo zitumia ikiwamo misaada zawadi na vitu ingine kama magari na   usa...

SIMBACHAWENE ATAKA URASIMU WA WATAALAMU USIDHOFISHE JUHUDI ZA SERIKALI

Image
Na   Mohamed Mhina wa Jeshi la POLISI- MPWAPWA Waziri wa Nchi Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mhe Simbachawene kikabithi kitabu cha Ilani ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa mwaka 2015-2020 Kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (w)Mpwapwa George Chigwiye.   Wataalam wa masuala ya fedha kwenye Halmashauri za Wilaya hapa nchini,   wmetakiwa kuacha urasimu wakati wa kufanya   maamuzi ya matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali katika kutekeleza miradi   ya maendeleo iliyokusudiwa. Agizo hilo limetolewa   na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. George Simbachawene, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe wakati wa hafla fupi ya kukabidhi taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 ya jimbo la Kibakwe kwa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dododma. Akikabidhi kitabu hicho chenye kurasa 34 kwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpwapwa Ndugu George Chigwiye, Mh. Simbachawene amesema kuwa baadh...

KAMATI YA MICHEZO MPWAPWA YAAHIDI KULETA MAPINDUZI YA MICHEZO

Image
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Mussa Shekimweri akiongea na kamati ya michezo haipo Pichani. MKUU wa wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma bwana Jabir Shekimweri   ameitaka kamati ya michezo ndani ya wilaya kuwa   daraja kati ya vilabu    na vyama vya michezo vya kiwilaya na kitaifa ili kuifanya Mpwapwa kuweza kurudi tena katika ulimwengu   wa Michezo. Shekimweri aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua kamati ya michezo ya wilaya ofisini kwake.    Katika nasaha zake Mkuu wa wilaya kwa kamati hiyo alisema Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya zilizokuwa zikitamba katika   ulimwengu wa michezo na kuwa na timu kama   Waziri mkuu,Mjimpwapwa, na timu zingine za madaraja ya chini . Alisema siku za hivi karibuni   Mpwapwa imekuwa   haifanyi vizuri katika sekta ya michezo kutokana na sababu nyingi za   kimtambuka. Alisema moja ya sababu zinazoidhofisha michezo Mpwapwa baadhi ya viongozi wa vyama na vilab...

WANANCHI IGOVU WAHAMASISHANA KUFANYA MAENDELEO

Image
Na Stephen Noel.  Wananchi wa Mtaa wa Igovu kaskazini wakimsikiliza Mwenyekiti wao wa mtaa baada ya kumaliza shughuli za maendeleo. WANANCHI wa Mtaa wa Igovu kata ya Mpwapwa mjini   Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma   wameushauri uongozi wa serikali za mitaa ngazi ya halmashauri kuweza kushirikiana na uongozi ngazi ya mitaa kutumia rasimali walizonazo   kuondoa chanagamoto   ndogondogo zinazowakabili wananchi kuliko kutegemea bajeti    ya serikali kuu. Wananchi hao walitoa ushauri huo   walipokuwa wakiongea na mwandishi wa habari    jana walipokuwa katika shughuli   za maendeleo za mtaa wa Igovu   kwa kuchimba barabara na   kuweka kufusi   ili kuweza kurahisisha upitakaji wa   njia mtaani   hapo. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mtaa huo bwana Elieza Mwaluko alisema kwa sasa seikali   ina miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa “lakini serikali ngazi ya halmashauri na serikali za mit...