SIMBACHAWENE ATAKA URASIMU WA WATAALAMU USIDHOFISHE JUHUDI ZA SERIKALI
Na Mohamed Mhina wa Jeshi la POLISI- MPWAPWA
Waziri wa Nchi Mambo ya Ndani na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe Mhe Simbachawene kikabithi kitabu cha Ilani ya utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa mwaka 2015-2020 Kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (w)Mpwapwa George Chigwiye.
Wataalam wa masuala ya fedha kwenye Halmashauri
za Wilaya hapa nchini, wmetakiwa kuacha
urasimu wakati wa kufanya maamuzi ya
matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo iliyokusudiwa.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh.
George Simbachawene, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kibakwe wakati wa hafla
fupi ya kukabidhi taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya
mwaka 2015-2020 ya jimbo la Kibakwe kwa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Mpwapwa
mkoani Dododma.
Akikabidhi kitabu hicho chenye kurasa 34 kwa
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mpwapwa Ndugu George Chigwiye, Mh. Simbachawene amesema
kuwa baadhi ya watendaji kwenye halmashauri za wilaya wamekuwa wakichelewesha michakato
ya utoaji wa fedha hizo na hivyo kusababisha ucheleweshwaji wa miradi ya huduma
kwa wananchi.
Mh.
Simbachawene pia amesema kwa upande wake, ametekeleza kwa mujibu wa ahadi alizo
ahidi kwa mwaka 2015 ametekeleza ilani
hiyo kwa zaidi ya asilimia 100% katika
sekta ya afya ,elimu,miundo mbinu ,nishati na
huduma za jamii.
Alisema pamoja na kutekeleza ilani hiyo
lakini pia anakerwa na urasimu unaofanywa
na watendaji wa halmasahauri ambao
wamekuwa wakisuasua katika
kuidhinisha malipo kwenda
kutekeleza miradi ya maendeleo kupitia fedha za mfuko wa jimbo
ambazo kimsingi zinakabidhiwa kwa halamashauri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
“Mfano fedha za kituo cha afya Pwaga nilizotoa
kutoka mfuko wa jimbo kutengeza fenicha za kituo cha hicho tangu septemba mwaka
2019 lakini zilikuwa hazikutolewa kwa kwa wakati
huku watalaamu wakidai watumie
mfumo wa ushindani kwa makandrasi.” amesema Simbachewene.
Kwa mujibu wa kitabu chake cha utekelezaji wa ilani ya CCM kwa mwaka 2015 -2020 Simbachawene
amesema kupitia serikali ya awamu ya
tano waliweza kuchonga barabara ambazo tangu uhuru viiji hivyo havijawahi kuwa na
barabara zinazopitika kwa nyakati zote.
Kwa uapnde wa elimu Mhe Simbachawene alisema, miodombinu ya majengo ya shule za
mingi na sekondari yameboreshwa yakiwemo mabweni na
vyumba vya madarasa.
Alisema
kwa muda mrefu Jimbo la Kibakwe
lenye tarafa mbili kata 18 na
vijiji 68 na vitongoji 322 lilikunyuma
katika upatikanaji wa hudama za jamii kama miundo mbinu ya barabara
,umeme maji zahati na vituo vya afya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wilayani Mpwapwa George
Chigwiye alisema alisema taarifa ya utekelezaji wa ilani hiyo utawasaidia kutadhimini kazi alizo
zifanya Mbunge wa jimbo la Kibakwe katika kukisaidia chama na kupunguza chanagamoto za maendeleo katika
jimbo lake la kibakwe.
Naye Katibu wa CCM wilayani Mpwapwa Jackson
Shalluah, amesema kama msimamizi wa
Ilani katika wilaya ya Mpwapwa ameridhishwa kwa kiasi kikubwa na utekelezaji
wa ilani katika jimbo la kibakwe
na hivyo kupelekea Chama Cha Mapinduzi
kuendelea kuaminiwa na wananchi .
MWISHO
Comments
Post a Comment