WAGOMBEA WAKUMBUSHWA KUJIEPUSHA NA RUSHWA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA UCHAGUZI.


. Mpwapwa.

 Mkuu wa Tasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa wilayani Mpwapwa Bi Julieth Mtuy akiwakumbusha madiwani wa Halmashuri  ya Mpwapwa juu ya sheria ya Uchaguzi.





 Mpwapwa
Mkuu  wa tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani Mpwapwa  mkoani Dodoma  Bi Julieth Mtuy  amewatahadharisha  wanasiasa wanao taka kuwania  nafasi za ubunge na udiwani katika  Majimbo ya   Mpwapwa  na Kibakwe kutojihusisha  na vitendo vya rushwa wakati wa kuelekea katika chaguzi   mkuu.

Mtuy ameyasema hayo na kuwakumbusha wagombea wa vyama vyote  kuto jihusisha na vitendo vyovyote vya utaoji wa rushwa kushawishi au kumchafua  mgombea mwenzie kama inavyo elekeza sheria ya gharama za uchaguzi namba 6 ya 2010 kuanzia kifungu 15,21-23 kinachomtaka mgombea kuweka wazi ghalama za uchaguzi  atakazo zitumia ikiwamo misaada zawadi na vitu ingine kama magari na  usafiri mwingine.

Mtuy alisema bila kufanya hivyo  mgombea  atakuwa amevunja sheria hiyo na atatakiwa kuchukuliwa  hatua za kisheria  ikiwamo kufikishwa mahakamani.

Aidha  amesema ameamua kuwakumbusha wagombea hao wakati wa kuelekea katika uchaguzi mkuu  kama wajibu wao ndani ya  tasisi kwa ajili ya kutoa elimu na kudhibiti vitendo vyote vya rushwa.

Hata hivyo alidai kuwa “ kipindi hiki kina mihemuko mikubwa kwa wagombea na wapambe wao hivyo nimewakumbusha  sheria ya kuzuia na kupambana  na  rushwa namba 11, ya 2007sheria ya uchaguzi namba 1ya mwaka 1985   na  sheria ya gharama za uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010  haionegi mtu wala kuangalia cheo chake au chama atokacho” amesisitiza

Hata hivyo alisema kila mwanaiasa anawajibu wa kufuata kanuni za chama chake juu ufanyaji kampeni,uchukuaji wa fomu na kutangaza nia . 

Hata hivyo amewataka wananchi  kutoa taarifa za vitendo vyote vinavyo ashiria utoaji wa Pesa au zawadi yeyote   ili waweze kuchukua hatua kwa muhusika.

MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.