WANANCHI IGOVU WAHAMASISHANA KUFANYA MAENDELEO
Na Stephen
Noel.
Wananchi wa Mtaa wa Igovu kaskazini wakimsikiliza Mwenyekiti wao wa mtaa baada ya kumaliza shughuli za maendeleo.
WANANCHI wa Mtaa wa Igovu
kata ya Mpwapwa mjini Wilaya ya Mpwapwa
mkoani Dodoma wameushauri uongozi wa
serikali za mitaa ngazi ya halmashauri kuweza kushirikiana na uongozi ngazi ya
mitaa kutumia rasimali walizonazo kuondoa chanagamoto ndogondogo zinazowakabili wananchi kuliko
kutegemea bajeti ya serikali kuu.
Wananchi hao walitoa
ushauri huo walipokuwa wakiongea na
mwandishi wa habari jana walipokuwa
katika shughuli za maendeleo za mtaa wa
Igovu kwa kuchimba barabara na kuweka kufusi
ili kuweza kurahisisha upitakaji wa
njia mtaani hapo.
Kwa mujibu wa
mwenyekiti wa mtaa huo bwana Elieza Mwaluko alisema kwa sasa seikali ina miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa
“lakini serikali ngazi ya halmashauri na serikali za mitaa ngazi ya mitaa na
vijiji wakitumia raslimali walizonazo watapunguza changamoto ambazo ni kero ya
maendeleo kwa wananchi”ameeleza.
Bwana Mwaluko amesema
kufuatia mvua kubwa zilozonyesha mwaka
jana zilisababisha barabara nyingi za
mitaani kuharibika na kusababisha adha
kwa wananchi wa mtaa huo ikiwemo
wagonjwa na misiba.
Pia amesema kutokana na kuharibika kwa barabara hizo
kulipelekea baadhi ya watu wenye magari kupaki magari yao kwa majirani kitu
alichokisema kuwa kilikuwa kinatishia usalama wa mali hizo.
Aidha Bwana Mwaluko
amesema wananachi hao wamehamasishana
wenyewe kwa wenyewe ili kuweza kuondoa
changamoto ya barabara katika mtaa wao ili kuweza kurahisisha mawasiliano kati ya mtaa na mtaa.
“Kwa sasa mji wa Mpwapwa
umekua kwa kasi kubwa kutokana na kufunguliwa kwa kituo cha JKT Hivyo tuna watu
wengi wenye magari lakini barabara
zilikuwa hazipitiki na hivyo iliwalazimu watu hao kuomba kupaki magari yao kwa
watu au sehemu za paking kitu kilichokuwa kinawaongezea gharama
lakini pia kufunguka kwa barabara hizi kutasaidia akitokea mgonjwa,mamamjamzito,
au msiba kuweza kumsafirisha kwa haraka tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa
inatulazimu kumbeka mgonjwa kwa kitanda hadi sehemu ambapo barabara ni nzuri”
aliongea
Mmoja wa Wananchi wa
mtaa huo na barozi wa wa mtaa wa Igovu
Kaskazini bwana Sospiter Magawa alisema majukumu ya serikali ya mitaa ni kuwajengea
uwezo wananchi kuweza kutambua majukumu madogo madogo kama ukarabati barabara ,kutoa nguvu
kazi ila wameiomba halmashauri kuweza kutoa magari kwa ajili ya kubeba vifusi na kokoto pindi zikihatika .
Bi Kathelini
Msalila amesema kutokana na kuharibika
kwa barabara hizo kulikuwa kunatishia
usalama kwa akina mama waja wazito
na wagonjwa pindi mgonjwa atokepo nykati za usiku .
“lakini wananchi
wakijitoa pia halmashauri utuunge mkono kwa
kupatia japo gari tu ili wananchi wajaze
mafuta lakini kila kitu
tukisubiri bajeti za serikali hatutafika na maendeleo yatachelewa sana Mpwapwa
lazima tujenge moyo kwa kujitoa kama wanavyo fanya mikoa mingine” ameongea Bi
Msalila.
Kwa upande wa ofisi
Tarura Wilaya ya Mpwapwa wamesema pamoja
na barabara hizo kuwa chini ya Tarura lakini wananchi wa eneo husika ndio
wamiliki wa barabra hizo kwa kuzilinda na kuzifanyia matengezo kama ya kufikia
mashimo na makorongo.
Hata hivyo amesema
changamoto inayo ikabili ofisi yao ni kukosa Loli na kusomba vifusi ili kuweza
kusaidia wananchi wanajitolea katika ukarabati mdogomdogo wa mitalo ya
barabara.
Mwishooo.
Comments
Post a Comment