KAMATI YA MICHEZO MPWAPWA YAAHIDI KULETA MAPINDUZI YA MICHEZO

Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Mussa Shekimweri akiongea na kamati ya michezo haipo Pichani.



MKUU wa wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma bwana Jabir Shekimweri  ameitaka kamati ya michezo ndani ya wilaya kuwa  daraja kati ya vilabu   na vyama vya michezo vya kiwilaya na kitaifa ili kuifanya Mpwapwa kuweza kurudi tena katika ulimwengu  wa Michezo.



Shekimweri aliyasema hayo jana alipokuwa akizindua kamati ya michezo ya wilaya ofisini kwake.  

Katika nasaha zake Mkuu wa wilaya kwa kamati hiyo alisema Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya zilizokuwa zikitamba katika  ulimwengu wa michezo na kuwa na timu kama  Waziri mkuu,Mjimpwapwa, na timu zingine za madaraja ya chini .

Alisema siku za hivi karibuni  Mpwapwa imekuwa  haifanyi vizuri katika sekta ya michezo kutokana na sababu nyingi za  kimtambuka.

Alisema moja ya sababu zinazoidhofisha michezo Mpwapwa baadhi ya viongozi wa vyama na vilabu kuto kufuata katiba zao  hivyo kupelekea migogoro ndani ya vilabu  na vyama  kitu kinachopelekea vilabu vingi kushindwa kuendela .

“ Natambua kuwa vilabu vingi na vyama  havifuati miongozo ya katiba  zinavyotaka na ndicho chanzo  cha migogoro ndani ya vyama  na vilabu hivyo nimewateuwa ili mkaweze kuangali hivyo vitu kama katiba ,utaratibu wa usajili, ukoje na je vyama vinafuata hayo alkini zaidi ya yote nataka mkawe daraja kati vilabu na  vyama vya kiwilaya na kitaifa” aliongea Shekimweri.

Pia  alisema  katika utafiti wa awali ametambua kuwa  baadhi ya vilabu na vyama uongozi wake umeisha muda lakini bado wako madarakani, kitu kinachosababisha migogoro na michezo kuto kuendelea mbele.

Aidha mkuu wa wilaya hiyo alisema  matarajio ya wilaya hiyo ni kuwa wilaya  amabyo watu wake  ni wenye utimamu wa mwili na  akili katika uzalishaji  kwa kushiriki katika michezo, na wilaya ya Mpwapwa kuweza kutambulika  kama kitovu  chenye  michezo  mbalimbali ulimwenguni.

Kwa upande Mwenyekiti wa kamati  ambae pia ni katibu Tawala wa wilaya hiyo Bi Sarah Ngalangasi amesema kamati imeyo imejipanga  kuleta mabadiliko ya kimichezo ndani ya wilaya ya Mpwapwa  na mkoa wa  Dodoma  kwa ujumla .

 Baadhi ya walimu wa michezo wilayani Mpwapwa wakiwa katika Mazoezi uwanja wa Shule ya Sekondari Mpwapwa.
 Amesema kamati hiyo itafuata  miongozo  na taratibu zote  ikiwemo  kuweka mpango  mkakati wa kamati hiyo juu ya uendelezaji wa michezo yote  ndani ya wilaya.

“Hii kamati imelenga  kuinuia michezo yote yaani sio mpira tuu hata bao,drafti,karata,na mpira wa miguu ,mpira wa Pete , na michezo yote ikiwemo ya jadi.” aliongea.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.