Posts

WANANCHI IGOVU WAHAMASISHANA KUFANYA MAENDELEO

Image
Na Stephen Noel.  Wananchi wa Mtaa wa Igovu kaskazini wakimsikiliza Mwenyekiti wao wa mtaa baada ya kumaliza shughuli za maendeleo. WANANCHI wa Mtaa wa Igovu kata ya Mpwapwa mjini   Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma   wameushauri uongozi wa serikali za mitaa ngazi ya halmashauri kuweza kushirikiana na uongozi ngazi ya mitaa kutumia rasimali walizonazo   kuondoa chanagamoto   ndogondogo zinazowakabili wananchi kuliko kutegemea bajeti    ya serikali kuu. Wananchi hao walitoa ushauri huo   walipokuwa wakiongea na mwandishi wa habari    jana walipokuwa katika shughuli   za maendeleo za mtaa wa Igovu   kwa kuchimba barabara na   kuweka kufusi   ili kuweza kurahisisha upitakaji wa   njia mtaani   hapo. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mtaa huo bwana Elieza Mwaluko alisema kwa sasa seikali   ina miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa “lakini serikali ngazi ya halmashauri na serikali za mit...

MAHAKAMA YA (W) MPWAPWA YAMFUNGA MIAKA 30 KWA KOSA LA KULIMA BANGI

Image
  MPWAPWA -MWANAWOTA. Mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya   ya Mpwapwa mkoa wa  Dodoma  imemuhukumu kifungo cha miaka 30   jela      bwana   Julius Lwagila (52) baada ya kupatikana na kosa   kulima   na kuhifadhi madawa ya kulevya aina ya bangi. Hukumu hiyo iliyokwishatolewa   mwaka  2019,na aliye kuwa hakimu mkazi wa mahakama hiyo bwana Paschal Mayumba lakini haikutekelezwa kutokana  na  mtuhumiwa siku ya hukumu   kutotokea mahakamani. Hata hivyo  mahakama ilitoa adhabu hiyo   bila mtuhumiwa huyo   kuwapo    mahakamani na mahakama kuamauru jeshi la polisi kumtafuta popote alipo ili atumikie adhabu yake.  Hukumu hiyo iliyotolewa na aliyekuwa   hakimu mkazi    wa Mahakam ya wilaya Mpwapwa   bwana Paschal Mayumba ambae kwa sasa amehamia mahakama ya   wilaya ya Dodoma.  Siku ya hukumu  hakimu Mayumba aliiambia mahaka...

WALIMU WATOA MSAADA KWA DC WA KUJIKINGA NA CORONA.

Image
MPWAPWA. Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akipokea ndoo za maji Tiririka   kutoka kwa katibu wa Umoja wa walimu ambao  ni wanachama wa CCM. UMOJA wa walimu wilayani Mpwapwa ambao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamekabidhi vifaa vya   kuji ki nga   na ugonjwa wa COVID 19 unaosabishwa na v irusi vya CORONA kwa mkuu wa wilaya hiyo. Vifaa hivyo vimepokelewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa. Katibu wa umoja huo   Mwl Nelson Nyaombo a me sema wameamua kufanya hivyo hili kuweza kuungana mkono na serikali katika jitihada kubwa wananazozifanya za mapambano dhidi ya Covid 19 hapa nchini na   ndani ya wilaya . M wl Nyaombo a me sema   vifaa walivyotoa ni ndoo 25 za maji tiririka   zenye thamani ya shilingi 300,000/=(laki tatu) ambazo serikali zitatoa muuongozo   njisi gani zitagawiwa .   A me sema walimu wananafasi kubwa   ya kuelimisha jamii   kwa njia ya   vitendo  ...

WAZIRI ZUNGU AWAPA MATUMANI WANA MPWAPWA.

Image
Waziri  wa mazingira  ofisi ya makamu wa Rais (M) na Mazingira Musa Azzan Zungu akielekea katika korongo la Shaban Robert  kuangalia uharibifu iliosababishwa na  korongo hilo(picha na Mpwapwa habari) WAZIRI mazingira   ofisi ya   makamu ya Rais Muungano na   na Mazingira Mussa Zungu(MB) amesema wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2020/2021 imetenga kiasi cha shilingi   billion 17.4 kwa ajili ya kupambana na uharibifu na mabadiliko ya Ikolojia. Waziri Zungu ameyasema hayo   wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma   alipokuwa kwenye ziara ya kikazi siku   ya moja ya kuona uharibifu wa mazingira   na uharibifu wa Korongo la Shaban Robert linalotishia maisha   ya wakazi wa wilaya hiyo   na miundo mbinu . Waziri   Zungu   amesema pamoja na mabadiliko ya tabia ya Nchi   lakini shughuli za kibinadamu    zimeiweka Mpwapwa   kuwa katika hali mbaya ya Kimazingira. “ Ofisini kwangu   kuna ta...

WATU WAWILI WAFA MAJI GULWE MTU NA MJOMBA YAKE

Image
 MPWAPWA -GULWE AJALI   Daraja la Gulwe walipokuwa wakioga hao Marehemu   WATU wawili Wakazi wa kijiji cha Gulwe wamefariki kufatia  kusobwa na maji   baada ya kudumbukia mtoni walipo kuwa wakioga   katika mto. Tukio hilo limetokea katika mto kinyasugwi   katika Kata ya Gulwe   wilaya ya Mpwapwa na mkoa wa Dodoma . Akielezea tukuio hilo Shuhuda wa Tukio hilo na diwani wa Kata ya Gulwe Bwana Gabriel Kazige   aliwataja watu wanaosadikiwa kufa maji kuwa ni Safari Matia(38)   na Maduo Msagati (12) mtu na mjomba   yake   wote wakazi wa Gulwe.   Wananchi wa kijiji cha Gulwe wakiwa Msibani baada ya kuupata miili ya marehemu. Aidha Bwana Bwana Kazige amesema   marehemu hao waleenda kuoga mtoni na ndipo   alipodumbuki kwenye maji     na mjomba mtu alipokuwa akitaka kumuokoa   “ wote wawili walizidiwa na maji   na kusobwa   nakufariki. Mhe Diwani alidai miili yo...