MAHAKAMA YA (W) MPWAPWA YAMFUNGA MIAKA 30 KWA KOSA LA KULIMA BANGI
MPWAPWA -MWANAWOTA.
Mahakama
ya hakimu mkazi ya wilaya ya Mpwapwa
mkoa wa Dodoma imemuhukumu kifungo cha miaka 30 jela bwana Julius
Lwagila (52) baada ya kupatikana na kosa kulima
na kuhifadhi madawa ya kulevya aina ya bangi.
Hukumu
hiyo iliyokwishatolewa mwaka 2019,na aliye kuwa hakimu mkazi wa mahakama hiyo bwana Paschal Mayumba lakini haikutekelezwa kutokana na
mtuhumiwa siku ya hukumu kutotokea
mahakamani.
Hata hivyo mahakama ilitoa adhabu hiyo
bila mtuhumiwa huyo kuwapo mahakamani na mahakama kuamauru
jeshi la polisi kumtafuta popote alipo ili atumikie adhabu yake.
Hukumu
hiyo iliyotolewa na aliyekuwa hakimu
mkazi wa Mahakam ya wilaya Mpwapwa bwana Paschal Mayumba ambae kwa sasa amehamia
mahakama ya wilaya ya Dodoma.
Siku ya hukumu hakimu Mayumba aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo mkazi wa kijiji cha Isasamambo kata ya
Mwanawota na wilaya ya Mpwapwa
alikamatwa na jeshi la polisi Mpwapwa likiwa katika oparesheni dhidi ya
madawa ya kulevya ambapo mtuhumiwa
alikamatwa akilima shamba la bangi lenye ukubwa wa heka tatu
na nusu.
Mwendesha
mashitaka wa polisi Bwana Willson Mwita
aliiambia mahakama kuwa “baada ya mtuhumiwa kutoroka kifungo jeshi la
polisi liliendelea kumtafuta na kufanikiwa kumkamata na kumfikisha mahakamani
ili atumikie kifungo chake”.aliongea
Alisema
katika shitaka la awali kesi hiyo namba 58 ya mwaka
2018 ilimuhusisha mtuhumiwa Julius Lwagila (52)kwa kosa la kulima na
kuhifadhi madawa ya kulevya kinyume na
kifungu namba 11(1)(a) na(2) cha sheria ya kuzuia madawa ya kulevya namba 5 ya mwaka 2015.
Hakimu Mfawidhi wa mahakama ya wilaya Bi
Nurupuldesia Nassary alimtaka mtuhumiwa aiambie mahakama kwanini hakutokea mahakani siku ya hukumu.
.
Akipewa
nafasi ya kujitetea mtuhumiwa aliiambia
mahakama kuwa “ Mimi sikutoroka ila kuna watu walinidanganya kuwa kesi yangu
imemalizika na wala nilikuwapo nyumbani tu sikuenda popote nashangaa kuja
kunikamata ” alijieleza.
Hakimu
Nassary alisema maelezo yake hayana mashiko hivyo anatakiwa kutumikia kifungo kilichotolewa na
mahakama hapo awali.
Mtuhumiwa
huyo aliiomba mahakama kumpatia hati ya nakala ya hukumu ili imsadie kukata
rufaa.
.Bwana Julius Lwagila akisindikizwa na polisi kwenye Mahabusu ya Mahakama akisuburi kwenda Gerezani baada ya kifungo chake kuthibitishwa na hakimu Mfawidhi.
Comments
Post a Comment