WALIMU WATOA MSAADA KWA DC WA KUJIKINGA NA CORONA.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Jabir Shekimweri akipokea ndoo za maji Tiririka kutoka kwa katibu wa Umoja wa walimu ambao ni wanachama wa CCM.
UMOJA wa walimu wilayani Mpwapwa ambao ni wanachama wa Chama
cha Mapinduzi (CCM) wamekabidhi vifaa vya
kujikinga na ugonjwa wa COVID 19 unaosabishwa
na virusi vya CORONA kwa mkuu wa wilaya hiyo.
Vifaa hivyo vimepokelewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa.
Vifaa hivyo vimepokelewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa.
Katibu wa umoja huo
Mwl Nelson Nyaombo amesema wameamua kufanya hivyo hili kuweza kuungana
mkono na serikali katika jitihada kubwa wananazozifanya za mapambano dhidi ya
Covid 19 hapa nchini na ndani ya wilaya .
Mwl Nyaombo amesema
vifaa walivyotoa ni ndoo 25 za maji tiririka zenye thamani ya shilingi 300,000/=(laki tatu)
ambazo serikali zitatoa muuongozo njisi
gani zitagawiwa .
Amesema walimu wananafasi kubwa ya kuelimisha jamii kwa njia ya vitendo kwa kuweza kutoa walicho nacho ili kuweza kusaidia watu ambao hawana uwezo wa kununua vifaa vya kujikinga na Corona.
Amesema walimu wananafasi kubwa ya kuelimisha jamii kwa njia ya vitendo kwa kuweza kutoa walicho nacho ili kuweza kusaidia watu ambao hawana uwezo wa kununua vifaa vya kujikinga na Corona.
Afisa Afya wa wilaya
Bi Mery Mabagwa amesema vifaa hivyo
vitasaidia sana katika mapambano ya ugonjwa huo katika maeneo yenye uhitaji zaidi .
Kwa upande wake mkuu
wa wilaya hiyo Bwana Jabir Shekimweri
amesema kuwa mchango huo utakuwa na tija kwa serikali wilayani Mpwapwa na kata zake kwa ujumla.
“ Natambua mchango huu katika harakati za kupambana na
ugonjwa huu lakini pia mara nyingi nikizungumza
na walimu nawaambia Taifa hili limejegwa na walimu Muasisi wa taifa hili alikuwa
mwalimu,Rais wa sasa pia ni mwalimu,
lazima walimu muwe mstari wa mbele kulipigania taifa hili kama walivyofanya na
wanavyofanya viongozi wa sasa wa taifa
hili kwa kuwa wazalendo, kujitambua na
kuitambua jamii mnayoifundisha inataka nini na kuacha kulalamika” aliongea
Aidha Shekimweri amesema
kwa kufanya hivyo inaonyesha kuwa watumishi wa umma tayari wanaonyesha kumuelewa
Rais wa Jamahuri wa Muungano katika utendaji wake.
Pia amesema uelewa wa corona kwa jamii ya Mpwapwa ni mkubwa kwa jamii kutumia maji
tiririka na vitakasa mikono na kuvaa barakoa pale amabapo kuna mkusanyiko
mkubwa wa watu kama makanisani
,sokoni na sehemu za kazi.
Walimu wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya hiyo Jabir Shekimweri.
Hata hivyo amesema jamii bado iendelee kuchukua
tahadhari na kuendelea kufanya kazi kwa bidii huku tahadhari zikuchukuliwa na
alitumia fursa hiyo kuwataka kada zingine za utumishi kuunga mkono jitihada za serikali
katika kupambana na ugonjwa wa COVID 19.
Mpaka sasa serikali imetangaza kuwapo kwa wagonjwa 480
walioambukizwa uginjwa huo na huku 168 kati ya wale wal
io ambukizwa wameshapona ugonjwa wa Corona.
mwisho.
Comments
Post a Comment