WATU WAWILI WAFA MAJI GULWE MTU NA MJOMBA YAKE
MPWAPWA -GULWE AJALI
Daraja la Gulwe walipokuwa wakioga hao Marehemu
WATU wawili Wakazi wa kijiji cha Gulwe wamefariki kufatia kusobwa na maji baada ya kudumbukia mtoni walipo kuwa wakioga katika mto.
Tukio hilo limetokea
katika mto kinyasugwi katika Kata ya
Gulwe wilaya ya Mpwapwa na mkoa wa
Dodoma .
Akielezea tukuio hilo
Shuhuda wa Tukio hilo na diwani wa Kata ya Gulwe Bwana Gabriel Kazige aliwataja watu wanaosadikiwa kufa maji kuwa
ni Safari Matia(38) na Maduo Msagati
(12) mtu na mjomba yake wote wakazi wa Gulwe.
Wananchi wa kijiji cha Gulwe wakiwa Msibani baada ya kuupata miili ya marehemu.
Aidha Bwana Bwana Kazige
amesema marehemu hao waleenda kuoga
mtoni na ndipo alipodumbuki kwenye maji na
mjomba mtu alipokuwa akitaka kumuokoa “
wote wawili walizidiwa na maji na
kusobwa nakufariki.
Mhe Diwani alidai miili
yote ya marehemu imepatikana na wanafanya mandalizi ya mazishi .
Pia shuhuda mwingine wa
tukio aliyejitambulisha kwa jina la Musa Willson amesema walikuwa wote mtoni bada ya kuona
wenzao wamezama na yeyealienda kuwaokoa alipo ona maji yanamzidi nguvu aliamua
kujiokoa mwenyewe.
“Mimi nilikuwa hapa nikawa
naangalia nikaona yule dogo alipoteleza maji yakamzidi akashidwa kuogolea mjomba mtu alivyo ona alitaka kumuokoa lakini
naye maji yakamzidi wote wakapelekwa kwenye kina kirefu na kufariki”
aliongea bwana Willson.
Hata hivyo viongozi wa kata hiyo wanadai kwa mwaka huu tayari mto huo umeshauwa watu saba kwa kuzama maji.
Comments
Post a Comment