WAZIRI ZUNGU AWAPA MATUMANI WANA MPWAPWA.
Waziri wa mazingira ofisi ya makamu wa Rais (M) na Mazingira Musa Azzan Zungu akielekea katika korongo la Shaban Robert kuangalia uharibifu iliosababishwa na korongo hilo(picha na Mpwapwa habari)
WAZIRI mazingira
ofisi ya makamu ya Rais Muungano
na na Mazingira Mussa Zungu(MB) amesema
wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2020/2021 imetenga kiasi cha shilingi billion 17.4 kwa ajili ya kupambana na
uharibifu na mabadiliko ya Ikolojia.
Waziri Zungu ameyasema hayo wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma alipokuwa kwenye ziara ya kikazi siku ya moja ya kuona uharibifu wa mazingira na uharibifu wa Korongo la Shaban Robert
linalotishia maisha ya wakazi wa wilaya
hiyo na miundo mbinu .
Waziri Zungu amesema pamoja na mabadiliko ya tabia ya Nchi
lakini shughuli za kibinadamu zimeiweka Mpwapwa kuwa katika hali mbaya ya Kimazingira.
“ Ofisini kwangu kuna
taarifa ya hili korongo kuwa linatishia
usalama wa maisha na makazi ya watu
pamoja na miundo mbinu ikiwamo madaraja ambayo yamesobwa lakini pia Mbunge wenu amekuwa akilipigia kelele sana korongo
hili” aliongea Wazir Zungu.
Aidha Waziri Zungu
amesema wizara yake katika kupambana
na uharibifu wa mazingira na
mabadiliko ya kiikolojia wizara hiyo
imetenga kiasi cha shilingi billion
17.4 ambazo zitatekeleza miradi
5 ya mazingira Tanzania bara na visiwani ambapo alisema mine itakuwa
Tanzania bara n mmoja utatekelezwa Nzanzibar kaskazini.
Pia waziri Zungu ametumia
fursa hiyo kutoa maagizo kwa viongozi wa
wilaya ya Mpwapwa kuendeleza usimamizi
na utunzaji wa mazingira na kuwatoa hofu wananchi wa wilaya hiyo kuwa
miundo mbinu ya madaraja iliyo bomoka
italejeshwa kwa wakati ili kurudisha mawasiliano.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir Shekimweri akitoa maelezo kwa Waziri wa mazingira.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabir
Shekimweri amedai ofisi yake
kwa kuishirikiana na ofisi Baraza la Mazingira(NEMC) Kanda ya kati wamefanya
tadhimi ya awali ya kuweza
kujua ghalama zitakazo weza kutumika kupunguza athari za korongo hilo kuwa ni zaidi
ya billion mbili.
Aidha Shakimwei ameongeza kuwa chanzo cha uharibifu wa
mazingira unaondelea katika milima ya
Kibolian na kwa Mdyanga.
“Mhe waziri uharibifu mkubwa wa mazingira unatokana na watu
kuvamia vilele vya milima na kufanya makazi ya kudumu huko lakini baada ya
kufunguliwa kwa kikosi cha jeshi huko juu kumesaidia kidigo kurudisha hali ya
kawaida” aliongea Shekimweri.
Pia mkuu wa wilaya amesema
baada ya madaraja kubomoka Ofisi ya Tanroad mkoa wa Dodoma inajenga daraja la mchepuko ili kuweza
kurudisha mawasilino yaliyokuwa wamekatika
katika mji wa Mpwapwa wa magari makubwa.
Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa George Lubeleje amesema kuwa kwa
sasa hali ya korongo lilipofikia ofisi ya Mkurugenzi hailiwezi tena bali
serikali kuu iingilie kati kuwanusuru wakazi wa mji Mpwapwa.
Meneja wa TARURA Mpwapwa mwandisi Emanuel Lukumai amesema ofisi yake tayari imeomba bajeti
ndogo kwa ajili kujenga daraja la muda la watembea kwa miguu na wameomba kiasi
cha shilingi million 457 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la kudumu.
.
Comments
Post a Comment