UFISADI WA KUTISHA MAPATO HALMASHAURI YA MPWAPWA
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma bwana Jabir Shekimweri amewapa masaa 6 ya kujieleza kwa barau kwa watendaji wa kata na vijiji kutokana kuto wasilisha fedha za mapato ya ndani jumla ya shilingingi milioni 84,202500/=kama mapato ya mwezi January . Shekimweri ametoa agizo hilo katika kikao cha baraza la madiwani kilicho fanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa halmasahauri. Shemweri kuna dalili za udanganyifu mkubwa ulipo kwa watendaji wa halmasahauri na watendaji wa kata katika ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mfumo maluumu wa mashine zijulikanazo kama POS. Aidha Shekimweri amedai serikali ikiwa katika harakati za kuboresha mapato kuimarisha uchumi wa wilaya kuna baadhi ya watendaji wa serikali wasio waaadilifu bila uwoga wamekuwa wakihujumu mapato ya halmashauri hiyo na kuifanya halamasahuri hiyo kuto kusonga mbele. “Ikiwa kama Ilani yetu ya kusimamia uwajibika...