TANZANIA YA KESHO INATISHIWA NA WIMBI LA WATOTO WA MITAANI.
IMEELEZWA kuwa tunaweza kuitengeneza Tanzania ya kesho kwa kuwekeza katika masalahi mapana ya watoto kimaadili,kiuchumi ,kielimu. Kauli hiyo ilitolewa na mkurugenzi mtendaji wa kituo cha kompasheni namba TZ 236 KKKT bwana Mboka Mwaipopo alipkuwa akiongea na waaandishi wa habari ofisi kwake hivi karibuni. Bwana Mboka alisema kuwa kumekuwako na vituo hivyo vilivyo anzishwa chini ya makanisa vikiwa na lengo la kuwalea watoto katika Nyanja za kielimu, kiroho na kiuchumi ili waweze kuwa wazalishaji na kuwezesha kuifikia Tanzania viwanda . Aidha Mboka alisema kuwa siku zinavyo zidi kusonga mbele kuna kunazidi kuongezeka kwa watoto wanaojulikana kama watoto wa mitaani kitu alicho kisema kuwa kinatishia ustawi wa taifa lolote siku za mbeleni. “Hiki ni kizazi cha watanzania wa Tanzania ya kesho tukiendelea kuwaita watoto wa mitaani tutambue kuwa Tanzania ya kesho n...