WAZIRI WA JK APATA PIGO AFIWA NA NDUGU 13 KWA MPIGO,MPWAPWA YAZIZIMA.

Na Stephen Noel-Mpwapwa.
WATANZANIA 13( kumi na watatu) wamefariki dunia nchini Uganda  walikokuwa wameenda kwenye harusi  ya binti yao baada ya gari gari lao kugongana  na loli karibu na mto  Katonga barabara ya Masaka  usiku wa kuamkia  tarehe 18septemba mwaka huu .
Gari hilo lenye namba T 540 DLC  mali ya Gregory Teu lilikuwa likuwarudisha Wanzania wa familia yake, walio wakirudi Tanzania kutokea Uganda, Teu aliyekuwa mbunge wa jimbo la Mpwapwa mstafu na naibu waziri wa Viwanda na Biasharakatika serikali ya awamu ya nne bwana Gregory Teu.
Kwa mujibu wa  taarifa kutoka katika ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Uganda zinasema  watanzania hao walikwenda nchini humo tangu tarehe 16 septemba mwaka huu kwa ajili ya  harusi ya  mtoto wake  bwana Gregory  Teu Mkazi wa Dar es salaam nchini Tanzania aliye olewa nchini Uganda .
Aidha taarifa hizo zinasema  gari hiyo ilikuwa na abilia 19 ambapo abilia 13 walifariki papo hapo na wengine sita kujeruhiwa   na kukimbizwa katika  hospitali ya Nsambya nchini Uganda.
Naibu balozi wa Tanzania nchini  Uganda  bwana Maleko amesema  kuwa chanzo cha ajali hiyo ni loli kupasuka taili na kupoteza muelekeo na kwenda kugongana na coster mali ya Bwana Gregory Teu.
Akiwataja watu walio fariki ni  bwana Sakazi Teu ,Mazengo George ,Alfred  Teu, Ester Teu , na Rehema Teu, wengine ni  Happy Soka, Digna,Einoth Laizer, Vivian  Mchaki, Edwin Kimaryo, Bony Njenga, Aristarik Shayo na Shangazi wote ndugu zake mbunge huyo mstaafu wa Mpwapwa  bwana Gregory Teu.
Akiwataja majeruhi walio walio jeruhiwa katika katika ajali hiyo Erasto Teu,Bon Mhilu na Dativa Boni.
Picha ya ajari liyo tokea nchini uganda ikionyesha njisi Magari yalivyo Gongna.

Msemaji wa ukoo wa teu wilayani Mpwapwa bwana   Stanely Mbijili amesema kuwa kuhusu utaratibu wa mazishi utafanyika mala baada ya ya miili ya marehemu kuwasili Tanzania “kwa sasa bado hatujapanga utaratibu wa mazishi uweje bali tunasubiri miili ifike Tanzania ndipo tupange itakuwaje maana imehusisha familia mbili  alitoa machozi’’ alieleza  Mbijili
Jamii yazungumzia  tukio hilo..
Mji wa mpwapwa na viunga vyake ukiwa umegubikwa na  na simanzi kubwa juu ya tukio hilo  baadhi ya watu walitolea maoni tukio na Kedmon Manyesela alisema  kifo ni Mpango wa  Mungu  hivyo  hakuna la kuweza  kuhoji wala kujiuizauliza ‘’ kwa sisi watu wa dini tunaamini kuwa kifo hakikimbiwi  hivyo kama kilipangwa kimepagwa   sasa tutasemaje juu ya hilo ndo imetokea basi”aliongea mmoja  wa wakazi wa Mpwapwa.
SERIKALI MPWAPWA YATOA TAMKO.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana Jabiri shekimweri amesema wanaungana na raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt Pombe Magufuli  kuwapa pole familia ya Teu kwa kuondokewa na wapedwa wao na aliwataka wafiwa kuwa na subira  kwenye kipindi hiki kigumu.
Aidha Shakimweri amesema msiba huu umegusa jamii ya wana Mpwapwa   na hivyo kuwataka wana Mpwapwa kuweza kujitoa kuwafariji wafiwa na  kutoa misaada ya hali na mali ili kuweza kufanisha mazishi ya marehemu hao.
Wazee wa jadi wazungumza.
Wakati huohuo baadhi ya wazee jadi mjini hapa  walisema kuwa mmoja wa wana ukoo  ambae ni Alfred Teu( Ntemi)alikiona kifo chake wiki mbili kabla ya kusafiri  maana kabla ya safari hiyo aligawa uridhi kwa wanawe wote kabla hajafariki kitu walicho kisema kuwa ni kinyume na utaratibu wa mila za kigogo.
Mzee ntemi wiki mbili kabla hajafariki alisha gawa pinde(urithi na mambo ya kijadi)  kwa mwanae  aliyejulikana kwa jina la Regino Teu  alipo ulizwa kuhusu kwanini anafanya hivyo alidai kuwa kaamua kufanya hivyo ili kuja kupunguza  migogoro kwa wanae wakati akisha kufa.
“Tulimuliza je ikitokea huyo unae mkabidhi Pinde akitangulia kufa kabla yako itakuwaje na pinde litakuwa la nani? alijibu hicho kitu hakiwezekani  na mimi ndio niliye amua niachane ambapo alichinja Ng’ombe na Mbuzi  na kufanya sherehe kubwa kitu alicho ashilia kifo”aliongea mmoja wa wazee wa jadi.
Kwa sasa maandilizi ya kupokea maiti hizo kutoka Uganda yanafanyika nyumbani kwa marehemu George Teu mtaa wa Hazina kata ya Vighawe mjini hapa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.