DC PANGANI AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUWAOMBEA.
.
Mkuu wa wilaya ya Pangani mkoani Tanga Bi Zainabu
Abdalah amewataka viongozi wa Dini
na watanzania wote kote nchini kuweza kumuombeombea Raisi ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,
John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wote
ili kuweza kuafanikiwa katika vita kubwa ya kiuchumi wanayo pambana
nayo.
Sambamba na hili Bi Zainabu
amewataka akina mama wote kuweza kuwasomesha watoto wa kike
ambao ndio kundi kubwa linalo adhiliwa na haki ya kunyimwa fursa za elimu kutokana na chanagamoto lukuki
zinazo wakabili watoto wa kike.
Bi Zainabu aliyasema hayo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma alipokuwa akiongea na wananchi wa wilaya hiyo
alipokuwa akihudhuria msiba wa mama mzazi wa
mkurugenzi wa halmasahauri ya Pangani
bwana Sabasi Chambasi ambae ni mzawa wa Mpwapwa.
Mkuu wa wilaya huyo bi Zainabu akiwa ndiye mkuu wa wilaya pekee mwenye umri
mdogo katika wakuu wa wilaya wote hapa nchini alisema “mimi pia ni mtoto wa
kike hivyo natambua changamoto zinazo
wakabili watoto wa kike wengi kushidwa kufikia ndoto zao kutokana na uhaba wa hudumaza jamii kama
afya,Elimu, na maji lakini pia mila na desturi zetu za kumtenga motto wa kike
pamoja na huduma uhaba wa huduma za
jamii zinazo mgusa moja kwa moja mwananmke” aliongea.
Mkuu wa wialya ya Pangani Bi Zainabu Abdalah akiwa katika msiba Mpwapwa.
Aidha alisema serikali ya awamu ya tano imepania kutetea
rasilimali za watanzania zikiwemo
madini,wanayama ,poli pamoja na matumizi sahihi ya fedha za umma ili ziweze
kuwa na tija kwa watanzania wote .
“tunaomba tumuombee
sana Raisi wetu ili avuke katika
vita hii lakini pia ninyi maparoko
tunaomba mtusaidie sana kulifanya taifa hili kwa kutuombea sana kwa maana tunavita kubwa
ambayo inakusa maslahi ya watu waliokuwa wamejilimbikizia mali za watanzania
kama zao hivyo hii ni vita ya kiuchumi tuombeeni sana”aliongea pia.
Alisema endapo rasimali za watanzania zikatunzwa zitawezesha
kuimarika kwa huduma za afya
,maji,pamoja na elimu ili kuweza kupata taifa
linaloweza kukidhi katika ushandani wa ajira na kuwezesha Tanzania
kuingia katika serikali ya viwanda.
Kwa upande wake paroko wa kanisa katolilki parokia ya Makle alieongoza
misa hiyo Padre Gaitano Mwaswenya
aliwataka watanzania kuacha kubaguana kwa ajili ya dini,ukabila pamoja na vyama vya siasa ambavyo
vinaonyesha dalili ya tabia hiyo kuanza kutamalaki katika taifa lililojengwa katika misingi ya umoja,
Padre Mwaswenya alisema
kusudi la Mungu kwa binadamu ni
upendo kati ya binadamu na binadamu
mwezie pia upendo kwa mungu ili taifa liwe na umoja na kuondoa tofauti zilizopo kati yetu zinazo
sabaishwa na utafauti wa dini,ukabila ,na vyama vya siasa.
Kwa upande wake Mbunge wa
wa Pangani bwana Juma Aweso alisema akina mama wakisimama katika
malezi na kutekeleza wajibu wao watalisaidia taifa la Tanzania kuimarika kwa
maadili katika jamii,
Pia Aweso alimtaja
Marehemu Ritha Sengimba Kama mama
shujaa kwa malezi ambae alikuwa na elimu ya kawaida lakini aliweza kuwasomesha watoto wake ambao
wana tija kwa taifa lote la Tanzania
hivyo alitoa wito kwa wazazi wekeza katika elimu kwa watoto wao ili wawe na tija kwa taifa lote la Tanzania.
Comments
Post a Comment