GEREZA LA MPWAPWA LAKABILIWA NA UHABA WA NYUMBA.
Gereza la Mpwapwa mkoani Dodoma
linakabiliwa na uhaba mkubwa wa nyumba za askari na kusababisha askari kukaa
kwenye nyumba ndogo na zisizo na hadhi kwa askari hao.
Haya yamebainishwa na Mkuu wa
gereza la mpwapwa mrakibu mwandamizi wa jeshi la magereza bwana Joseph Tembo
ameanza jitihada za kupunguza uhaba wa nyumba za askari kwa kuwatumia wafungwa
kufanya kazi hizo.
Bwana tembo amesema kuwa mpaka
sasa wamefyatua na kuchoma zaidi ya tofali elfu harobaini na tano ambazo
zitatumika kujengaea nyumba sita za watumishi gereza hilo,Tembo amesema
serikali inazitaka magereza kuwa sehemu ya kuwabadilisha tabia na mtazamo kwa
wafungwa wale wanao kinzana na sheria .
Mkuu wa Gereza la Mpwapwa Joseph Tembo akizungumzia hali halisi ya Mkakati wa Uboreshaji wa nyumba za Askari.
Adha amesema kukamilika kwa nyumba
hizo kutapunguza adha ya nyumba kwa askari kumi nambili kupata makazi bora na ya kisasa ambapo hapo awali walikuwa wanatumia
nyumba za matope na dogo ambapo zolikuwa zinapelekea msongamano kwa maskari hao
hasa kwa wenye familia kubwa na, kuongeza kuwa tayari washachimba misingi ya
nyumba mbili ambazo ujenzi wake utaanza hivi punde na lengo la gereza hilo ni
kufyatua tofali laki moja na elfu hamsini.
Comments
Post a Comment