DC atangaza vita na waharibifu wa mazingira mpwapwa.
Mkuu wa wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma Jabir Shekimweri ametangaza vita na watumishi wa serikali watakao bainika katika kuihijumu serikali katika vita ya kupambana na uharibifu wa mazingira Mpwapwa. Shekimweri aliyasema hayo ofisi kwake alipo kuwa akiongea na waandishi juu mikakati ya kuikomboa wilaya hiyo juu ya uharibifu wamazingira. Mkuu wa wilaya hiyo alisema kupitia kamati ya ulinzi na usalama imebaini baadhi ya watumishi wa serikali wamekwa wakihusika katika uharibifu wa mazingira kwa kuwa na vibali feki ya kuchana mbao . Aidha alisema watumishi wote waliotuhumiwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kinidhamu na hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakama kujibu tuhuma zinazo wakabili. “Inasikitisha kuona watumishi wenzangu wa serikali kujikita katika sula la uharibifu wa mazingira ,kwa hili sitakuwa na uvumilivu hata kidogo katika mazingira mimi ni...