WATOTO 6041 WANATARAJIA KUFANYA MTIHANI WA KUHITIMU SHULE YA MSINGI MPWAPWA.



.
Jumla ya watahiniwa  6041 wa darasa la saba wilayani Mpwapwa mkoani hapa wanatarajia kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba  mwaka 2016
Kati ya watoto  hao wavulana  ni2654 na wasichana  3387 wakati walio anza  darasa la kwanza walikuwa watoto 7931 wakiwamo wasichana 4247 na wavulana 3684 mwaka  1999.
Ofisa elimu   talaaluma wilayani hapa bi Mery Chakupewa  alisema kuwa  wanafunzi walishidwa kufanya mtihani huo ni watoto 1890 ikiwamo sababu za kuhama , vifo, na utoro wa lejaleja .
Akifungua mfunzo ya usimamizi wa mtihani huo mkuu wa wilaya ya Mpwa[pwa bwana Jabil Shakimweri  aliwataka walimu hao kuto lubuniwa na kujiingiza katika vitendo vyote vya udanganyifu   kwa kumuonyesha mwanafunzi majibu au  kumfanyia mtihani.
Shakimweli alisema kuna baadhi ya walimu walijikuta na wakjiingiza katika viitendo hivyo vya udanaganyifu na kujikuta wanakabailiwa na matatizo makubwa  baada ya kubainika kukiuka taratibu za usimamizi wa mitihani  na baraza la mithani hapa nchini.
Aliwataka walimu hao kuweza kuwa waadilifu na kufuata   na maelekezo yaliyo tolewa na wakubwa wao wa kazi  na baraza la mitihani.
Aidha Shalimweli alisema kuwa siku hadi siku zinavyo zidi maadili ya  walimu wa kiume yanazidi kupungua na kuzidi kuongezaka kwa vitendo  walimu kuwapa mimba wanafunzi wao kitu alicho kisema kuwa katika wilaya yake hatapenda kukisikia  wala kukiona .
“Ukweli katik vitu ambavyo nina umilivu nvyo mdogo ni kusikia mwalimu kampa mimba mwanafunzi wake  kitendo hicho kinanikera hadi basi  na ninatamani mtu huyu akigundulika kuwa kweli  amefanya kosa hilo  afugwe kabis jela kwa mujibu sheria zinavyosema”aliongea mkuu wa wilaya Shakimweri.
Hta hivyo aliwataka walimu  wakuu na waratibu wa elimu kata kuweza kukaa vikao vya pamoja  juu ya kuyatatua na kuonyona katika ofisi zao kama kuna mwalimu ambae anajihusisha na suala hilo achane nalo kabisa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.