UVCCM ACHANE KUTUMIKA - KIMTENDE
Katibu wa jumuiya
ya umoja wa vijana wa vijana UVCCM wilwywni Mpwapwa mkoani Dodoma bwana Jumanne Kimtende amewataka
vijana kuweza kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za ndani ya chama ya hapo mwakani 2017.
Kimtende ameyasema hayo
jana ofisini kwake alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya
maandalizi ya kuingia katika chaguzi ndani ya chama znazo talajiwa kufanyika mwaka 2017 nchini kote.
Kimtende amesema kuwa
vijana wamekuwa walalamikaji wakubwa kuwa wamekuwa watu wa kufanyiwa maamuzi yanayo
wahusu na watu ambao sio vijana, kitu alicho kisema kuwa kinatokana na vijana
wenyewe kutojiingiza katika mfumo wa
kufanya maamuzi ambao ni ungozi ndani ya
chama na wao ubaki kutumiwa kuwanadi wagombea kitu alicho kisema kuwa vijan
wajitambue na waaache kutumika.
Aidha Kimtende amesema
kuwa lazima vijana wajiandae kuwanai nafasi mbalimbali ndani ya jumuiya
hiyo ili kuweza kukiweka chama katika msingi mzuri na ulio imara na dhabiti
ndani ya chama na serikali
Hata hivyo kimtemnde ametumia
fursa hiyo kumshukuru Rais wa awamu ya Tano Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuwaamini
na kuwapa majukumu ya uongozi
vijana mbalimbali katika seikali na tasisi zake.
Pia amesema viongozi vijana wote walio teuliwa raisi lazima
kuweza kuonyesha viongo vya juu vya uwajibikaji
ili raisi aendeee kuwa na imani na vijana na kuondoa dhana iliyo kuwa imejengeka
miongoni mwa jamii kuwa vijana ni taifa la kesho.
Akizungumzia migogoro inayo endelea katika vyama vya siasa
kimtende alisema lazima vyama hivyo kuweza kufuta katiba zao za vyama ili kuweza kuwa na amani katika vyama vyao.
Comments
Post a Comment