WANCHUO WAMTUMBUA MKUU WAO
SAKATA la la uwajibishwaji
kwa la viongozi wazembe likiwa linashika kasi katika tasisi mbalimbali
za umma na za serikali sasa limemkuta
mkuu wa chuo cha wanannchi Chisalu bwana
Sebastian Aweit kuvuliwa madaraka yake kwa muda na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kwa tuhuma mbalimbali.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni katika chuo cha wananchi Chisalu kilichopo
katika kata ya Matomondo wilayani Mpwapwa bala baada ya kamati ya ulinzi na usalama wilayani hapa
bwana Jabili shakimweli ambae ni mkuu wa
wilaya hiyo kummvua madaraka ya ukuu wa chuo kwa muda, mkuu wa
chuo cha maendeleo ya wananchi Chisalu
Bwana Sebastian Aweit kwa kushidwa kuongoza chuo hicho .
Shakimweli amesema amefikia uamuzi huo mala baada ya kuona na
kujiridhisha juu za tuhuma zilizotolewa na wanachuo wa chuo hicho hadi kupelekea
wanafunzi kugoma kuingia madarasani na
kutishia hali ya usalama wa wafanyakazi wa chuo hicho na mali za chuo .
Bwana Shakimweri amesema mkuu wa chuo hicho alikuwa analalamikiwa na wanachuo hao kuwa amekuwa
akiendesha chuo hicho kibabe bila kusikiliza malalamiko yao na kushidwa
kuitisha vikao vya bodi kwa zaidi ya
miaka miwili,na kushidwa kufuata miongozo ya uendeshaji wa vyuo vya maendeleo
ya wananchi.
Pia mkuu wa wilaya huyo amesema kwamba wanachuo wa chuo
cha maendeleo ya wanachi (FDC) lakini kwenye mitahani yao ya mwisho
ilikuwa inandaliwa na VETA kitu
alichosema kilizua mgogoro mkubwa kati
ya wanachuo na uongozi wa chuo hicho.
Aidha alisema kuwa pia
wanachuo wa chuo hicho pamoja na kufanya mitihani ya VETA lakini vyeti vyao
wakivipeleka kwenye soko la ajira
walikuwa hawatambuliki kutokana chuo chao kuto kuwa na hadhi ya kufanya
mitihani hiyo ya VETA.
Hata hivyo amesema kuwa
kuna baadhi ya kozi ambazo zilianzishwa chuoni hapo kama ya kilimo na
mifugo haijawi kufundishwa tangu zianzishwe lakini wanachuo ilikuwa inawalazimu
kujibia katika mitihani yao ya mwisho.
Amesema hata hivyo suala hilo ameichia bodi ya chuo hicho ili kuweza kuliwasilisha wizarani kwa
hatua zaidi.
Comments
Post a Comment