TEMBO AUWA MTU CHUNYU MPWAPWA



na noel stephen

SERIKALI imewaagiza wakurugenzi wa halmashauri, maafisa elimu wa mikoa
na wilaya nchini, pamoja na wakuu wa shule, kuhakikisha fedha
zinazotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Camfed linalojihusisha
na masuala ya elimu kutumika kwa malengo  yaliyokusudiwa.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini hapa, Naibu waziri ofisi
ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Elimu,
Kassim Majaliwa, alisema wizara imejipanga kuongeza juhudi za
ufuatiliaji wa fedha hizo ili kuhakikisha zinawafikia walengwa na
haitasita kuwachukulia hatua kali watakaotumia fedha hizo kinyume.

Alisema serikali tayari imeonyesha jitihada za kudhibiti fedha hizo
ambazo zinafanya kazi ya kuboresha elimu hususan kwa watoto wa kike.

Hata hivyo, alisema baadhi ya walimu wakuu ambao walibainika kuzitumia
fedha hizo kinyume na matakwa walisimamishwa kazi na wengine kushushwa
vyeo.

“Kwa mfano kwa aliyekuwa mwalimu mkuu wa nyamisati na mwenzie wa
kibiti tuligundua maeneo ambayo mtoto anapaswa kupewa fedha kwa ajili
ya mahitaji mengine lakini walimu hao walikuwa hawatoi,”alisema

Aidha, Naibu huyo, alisema tayari serikali imeweka mazingira mazuri
ili Camfed iweze kufanya kazi kwa umakini na usahihi katika kuiboresha
sekta ya elimu nchini.

Alitoa wito kwa taasisi mbalimbali na mashirika yasiyo ya kiserikali
yanayojihusuisha na elimu kutatua changamoto zilizopo kwa kushirikiana
na serikali.

“Camfed ni miongoni mwa taasisi zilizoingia kwa vitendo na imeshiriki
kikamilifu katika kutatua changamoto zilizopo,”alisema

Kwa upande wake Naibu waziri wa Tamisemi anayeshughukia serikali za
mitaa, Aggrey Mwanri, alilihakikishia shirika hilo kupata ushirikiano
wa kutosha kutoka katika wizara hiyo ili kuhakikisha walengwa
wananufaika na ufadhili huo.

Alisema katika hali ya kawaida shughuli hiyo ilipaswa ifanywe na
serikali lakini kutokana na jitihada za shirika hilo serikali
itaungana nalo ili kufikia malengo yake.

Alifafanua kuwa tayari shirika hilo limeshatumia bilioni tisa, kwakuwa
sasa watafanya kazi pamoja atahakikisha fedha hizo zinawafikia
walengwa.

Naye mkurugenzi wa shirika hilo nchini, Msaada Daudi Balula, alisema
shirika hilo makao makuu yake ni Cambridge uingereza ambalo mkurugenzi
muasisi wa shirika hilo ni Ann Cotton ambaye alianza kwa madhumuni ya
kusaidia watoto wa kike kupata elimu na kujipatia ajira.

Alisema shirika hilo limeweza kusaidia watoto 6,332 tangu mwaka 2005
kupitia mradi wa Bursary na watoto 64,227 kupitia mfuko wa dharura.

Alisema pia kumekuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na
tatizo la utoro na mimba kwa wafadhiliwa, kukosa ushirikiano kwa
wanajamii, ufaulu mdogo, na matumizi mabaya ya fedha za wafadhiliwa
yanayofanywa na baadhi ya wakuu wa shule.
a
Shirika hilo linafanya kazi katika wilaya za Bagamoyo, Iringa
vijijini, Morogoro vijijini, Handeni, Pangani, Kilombero, Kilosa,
Kibaha, Kilolo na Rufiji.
Mwisho.

na noel  stephen  mpwpwa
Mtu  mmoja aliyetambulika kwa jina la ZARAU MBUNI(27)  mkazi waya chunyu wilayani mpwapwa mkoani dodoma  ameuwawa kwa TEMBO  katika kata  hiyo
MKUU polisi wilayni mpwapwa JEREMIA SHIRA amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa  marehemu aliuwawa nov 2 mwaka huu katika kijiji cha msagali  kata ya chunyu wilayani mpwapwamajira ya saa kumi na moja jioni  kwa kukanyagwakanyagwa na tembo baada ya  tembo kuonekana  kijijini hapo, na wanakijiji kuanza kumshangaa na kumchezea huku wakimlushia maboga  na vitu vingine.
Shira  amesema kuwa kutokana  na tembo kuonekana katika kijijn hicho  na kuwa ni  mnyama  wa ajabu kijijini hapo na  baadhi ya wanakiji walianza kumchezea  na kumchokaza ndipo alipo mua  kijana huyu kwa kumkanyagakanyaga .
Naye Diwani wa kata hiyo  NEHEMIA KONGAWADODO ametoa lawama kwa watumishi wa  mali asili na utalii kuwa tembo huyo alianza kuonekana kijijini  hapo na kutoa taarifa hizo kuwa tembo anaonekana kijijini hapo  lakini   idara hiyo  bila kuchukua hatua zozote.
Aidha amedai kuwa  kuna uzembe unatokea kwa watumishi wa mali ya asili na utalii kupuuzia  taarifa za wanakijiji wakitoa  taarifa hizo" huwaji mpaka wasikie  kuna maafa  yametokea sasa  toka tarehe 29.0ctoba mwaka huu tumetoa taarifa  lakini baada ya kuwapigia  juu ya maafa ya kuuwawa kwa mkazi mmoja  wa kijiji hiki ndo wanakuja wanakuja kufanya nini sasa kushuhudia  kupotelewa kwa mkazi wetu  au  kuja kuuza sura tu hapa"alieleza
Pia Nehemia ameongeza kuwa wana game hao baada ya kutokea kuuwawa kwa bwana Zarau   ndipo  wanakuja kumatafuta tembo  baada ya kuleta maafa .
Kwa wilaya hii si mala ya kwanza  kwa maafa ya watu kujeruhiwa   na tembo  ambapo mala ya kwanza kijana  mlowe mkazi wa pwaga alijeruhiwa na tembo mwezi mmei mwaka huu  na kwasasa bwana Mlowe alikatwa mguu alio kuwa kajeruhiwa na tembo na sasa kusababishiwa  kilema cha maisha .

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.