CCM YAIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI WA UDIWANI MPWAPWA
na noel stephen
SERIKALI imewaagiza wakurugenzi wa halmashauri, maafisa elimu wa mikoa
na wilaya nchini, pamoja na wakuu wa shule, kuhakikisha fedha
zinazotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Camfed linalojihusisha
na masuala ya elimu kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini hapa, Naibu waziri ofisi
ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Elimu,
Kassim Majaliwa, alisema wizara imejipanga kuongeza juhudi za
ufuatiliaji wa fedha hizo ili kuhakikisha zinawafikia walengwa na
haitasita kuwachukulia hatua kali watakaotumia fedha hizo kinyume.
Alisema serikali tayari imeonyesha jitihada za kudhibiti fedha hizo
ambazo zinafanya kazi ya kuboresha elimu hususan kwa watoto wa kike.
Hata hivyo, alisema baadhi ya walimu wakuu ambao walibainika kuzitumia
fedha hizo kinyume na matakwa walisimamishwa kazi na wengine kushushwa
vyeo.
“Kwa mfano kwa aliyekuwa mwalimu mkuu wa nyamisati na mwenzie wa
kibiti tuligundua maeneo ambayo mtoto anapaswa kupewa fedha kwa ajili
ya mahitaji mengine lakini walimu hao walikuwa hawatoi,”alisema
Aidha, Naibu huyo, alisema tayari serikali imeweka mazingira mazuri
ili Camfed iweze kufanya kazi kwa umakini na usahihi katika kuiboresha
sekta ya elimu nchini.
Alitoa wito kwa taasisi mbalimbali na mashirika yasiyo ya kiserikali
yanayojihusuisha na elimu kutatua changamoto zilizopo kwa kushirikiana
na serikali.
“Camfed ni miongoni mwa taasisi zilizoingia kwa vitendo na imeshiriki
kikamilifu katika kutatua changamoto zilizopo,”alisema
Kwa upande wake Naibu waziri wa Tamisemi anayeshughukia serikali za
mitaa, Aggrey Mwanri, alilihakikishia shirika hilo kupata ushirikiano
wa kutosha kutoka katika wizara hiyo ili kuhakikisha walengwa
wananufaika na ufadhili huo.
Alisema katika hali ya kawaida shughuli hiyo ilipaswa ifanywe na
serikali lakini kutokana na jitihada za shirika hilo serikali
itaungana nalo ili kufikia malengo yake.
Alifafanua kuwa tayari shirika hilo limeshatumia bilioni tisa, kwakuwa
sasa watafanya kazi pamoja atahakikisha fedha hizo zinawafikia
walengwa.
Naye mkurugenzi wa shirika hilo nchini, Msaada Daudi Balula, alisema
shirika hilo makao makuu yake ni Cambridge uingereza ambalo mkurugenzi
muasisi wa shirika hilo ni Ann Cotton ambaye alianza kwa madhumuni ya
kusaidia watoto wa kike kupata elimu na kujipatia ajira.
Alisema shirika hilo limeweza kusaidia watoto 6,332 tangu mwaka 2005
kupitia mradi wa Bursary na watoto 64,227 kupitia mfuko wa dharura.
Alisema pia kumekuwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na
tatizo la utoro na mimba kwa wafadhiliwa, kukosa ushirikiano kwa
wanajamii, ufaulu mdogo, na matumizi mabaya ya fedha za wafadhiliwa
yanayofanywa na baadhi ya wakuu wa shule.
a
Shirika hilo linafanya kazi katika wilaya za Bagamoyo, Iringa
vijijini, Morogoro vijijini, Handeni, Pangani, Kilombero, Kilosa,
Kibaha, Kilolo na Rufiji.
Mwisho.
na noel stephen mpwpwa
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la ZARAU MBUNI(27) mkazi waya chunyu wilayani mpwapwa mkoani dodoma ameuwawa kwa TEMBO katika kata hiyo
MKUU polisi wilayni mpwapwa JEREMIA SHIRA amedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema kuwa marehemu aliuwawa nov 2 mwaka huu katika kijiji cha msagali kata ya chunyu wilayani mpwapwamajira ya saa kumi na moja jioni kwa kukanyagwakanyagwa na tembo baada ya tembo kuonekana kijijini hapo, na wanakijiji kuanza kumshangaa na kumchezea huku wakimlushia maboga na vitu vingine.
Shira amesema kuwa kutokana na tembo kuonekana katika kijijn hicho na kuwa ni mnyama wa ajabu kijijini hapo na baadhi ya wanakiji walianza kumchezea na kumchokaza ndipo alipo mua kijana huyu kwa kumkanyagakanyaga .
Naye Diwani wa kata hiyo NEHEMIA KONGAWADODO ametoa lawama kwa watumishi wa mali asili na utalii kuwa tembo huyo alianza kuonekana kijijini hapo na kutoa taarifa hizo kuwa tembo anaonekana kijijini hapo lakini idara hiyo bila kuchukua hatua zozote.
Aidha amedai kuwa kuna uzembe unatokea kwa watumishi wa mali ya asili na utalii kupuuzia taarifa za wanakijiji wakitoa taarifa hizo" huwaji mpaka wasikie kuna maafa yametokea sasa toka tarehe 29.0ctoba mwaka huu tumetoa taarifa lakini baada ya kuwapigia juu ya maafa ya kuuwawa kwa mkazi mmoja wa kijiji hiki ndo wanakuja wanakuja kufanya nini sasa kushuhudia kupotelewa kwa mkazi wetu au kuja kuuza sura tu hapa"alieleza
Pia Nehemia ameongeza kuwa wana game hao baada ya kutokea kuuwawa kwa bwana Zarau ndipo wanakuja kumatafuta tembo baada ya kuleta maafa .
Kwa wilaya hii si mala ya kwanza kwa maafa ya watu kujeruhiwa na tembo ambapo mala ya kwanza kijana mlowe mkazi wa pwaga alijeruhiwa na tembo mwezi mmei mwaka huu na kwasasa bwana Mlowe alikatwa mguu alio kuwa kajeruhiwa na tembo na sasa kusababishiwa kilema cha maisha .
Comments
Post a Comment