TASISI ZA MKOPO KIKWZO KWA WAJASILIA MALI WADOGO.

Na noel stephen dodoma
Tanzania kuna uwezekano mkubwa  wa kushidwa kufikia   baadhi ya  malengo yake milenium kutokana na changamoto zilizoonekana katika utekelezaji wa malengo hayo.
Akiongea na radio mwangaza fm mmoja wa wajasilia  mali  aliyejiatambulisha kwa jina la solomon Ambakisye alisema kuwa kuna chanagamoto kubwa  katika kulifikia lengo la tatu la milenium amabalo linadai kuondoa  umaskini wa  kipato  kwa mtanzania .
Ambakisye amedai kuwa   wajasilia mali wengi nchini   hawana elimu ya  riba na mikopo kwa tasisi za fedha kitu ambacho kinawapelekea  kujingiza kwenye madeni yenye riba kubwa amabayo  amesema kuwa badala ya kuwainua kiuchumi  bali inazidi kuwadidimiza kwa mikopo hiyo kuwa na riba kubwa.
Aidha amedai kuwa  bado serikali inatakiwa kulaumiwa kwa hili kutokana na kuweka malengo mengi   lakini kushindwa kuiwekea mikakati ya utekelezaji wa malengo hayo.
"Tanzania sisi ni mabingwa wa kupanga  lakini ni  wadhaifu katika utekelezaji wa malengo tunayao jipangia  kutokana  na kushuka kwa utawala  bora na uwajibikaji, serikali ingeweka chombo cha  kudhibiti hizi tasisi za fedha  kuliko ilivyo hivi sasa kila tasisi inajipangia riba yake na bila kuwa na udhibiti wowote"alisisitiza
Kwa upande wake afisa mikopo ya  tasisi ya kukopesha wajasilia mali wadaogo  ijulikanayo kama FINCA tawi la dodoma   Bi Retisia Mwakasitu amesema  katika mikopo yao hutoa mikopo ya aina mbili amabayo ni mkopo  wa mtu mmoja  na mkopo wa kikundi ambapo  mkopo  wa kikundi  hilipwa kwa asilimia 12-15 wakati mkopo wa mtu mmoja ni asilimia 9.5
Aidha  amedai kuwa wapo watu wanaoshidwa kulipa  madeni yao kwa wakati na  kikundi  wanachukua jukumu la kumlipia mwenzao ambae ameshidwa kulipa deni hili ua hulazimika kuuza samani zake   kuweza kulipa dhamana ya mkopo huo.
Pamoja na hayo Mwakasitu amewaasa wajasiliamali  waweze kusoma mikataba kabla hawajajaza  fomu ya mkopo ili kupunguza migongano wakati wa kulipa  deni.
MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.