WANAWAKE WAOBWA KUTAMBULIWA NA KATIBA
aNa noel Stephen mpwapwa
Mwenye kiti wa umoja wa wanawake Tanzania( UWT) wilayani Mpwapwa ZELLY NGOWO amesema kuwa anaomba katiba ijayo iweze kumtambua na kumlinda mwanamke kisheria na kikatiba juu haki zake za msingi na usawa mbele ya jamii,
Mwenyekiti huyo aliya sema hayo wilayani mpwapwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa jumuiya hiyo ulio fanyika mwishoni mwa wiki hii mjini mpwapwa mkoani dodoma
Bi Ngowo alisema kuwa yeye kama mwenyekiti ana mipango endelevu kwa akinamama na kusimamia haki kwa watoto kwani watoto wengi wanashindwa kuendelea na shule kutokana na kukosa haki zao za msingi za kutopelekwa shule.
Pia alisema wanawake wanaweza kusimamia miradi na kuendeleza miradi ndani ya kikundi kwa kupitia nyaja mbalimbali ili mradi wapatiwe elimu ya kutosha kwenye vikundi watakavyo jiunga kwani wanawake wakiwezeshwa wanaweza.
Bi ngowo alisema kuwa wanawake wengi ni waonga ndio maana wananyenyasika sana kwa sababu ya kushindwa kusimama wao kama wao na kufanya kazi kwa bidii ili waweze kujikwamua kiuchumi na familia zao
“Kwa sasa kama mimi mwenyekiti nina mpango endelevu wa kufungua shule ya kujifunza kushona yaani cherehani kwa wakina mama na wasichana ili wajifunze na kujipatia ajira yao na sio kukaa kutegemea kuletewa”
Alisema kuwa wakina baba wanatakiwa kuwaunga mkono wanawake zao kwa sababu wanawake wakiwezeshwa wanaweza kwanza wanaaminika na jamii kwanini wakina baba wanashindwa kuwaunga mkono wake zao ili waachane na hali ya kutegemea mwanaume na yeye anaweza kufanya biashara yoyote ile .
Bi ngowo alisema wanawake wote wanatakiwa kuwa kitu kimoja kwani umoja ni nguvu wanatakiwa kupendana na kusaidiana pale inapoonekana pana tatizo kwa mwingine na kuachana na hali ya roho mbaya kwa mfano ukiona mwanamke anagombea nafasi wanawake mnatakiwa kuumunga mkono ili apite kwenye ile nafasi baadae atawasaida wanawake wenzie ’’
Alisema kuwa kwa sasa kuna nafasi nyingi za kugombea au kuteuliwa wanawake acheni hali ya kuongopa jitokezeni kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali na kuachana na hali ya kutegemea mume zao kwani maisha ni magumu sana tafuteni maisha na kupeleka watoto shuleni na sio kuwaozesha bado wadogo waende shule elimu ni mwanga wa jamii kwa mtoto.
Comments
Post a Comment