VYANZO VYA MIGOGORO YA ARDHI NCHINI
NA NOEL STEPHEN MPWAPWA
Imegundulika kuwa migogoro mingi ya ardhi hapa nchini inasababishwa na vijiji vingi kukosa mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Hali hiyo imegundulika na mwandishi wetu aliyeko wilayani mpwapwa aliyefanya utafiti juu ya kugundua chanzo cha migogoro mingi inayotokea kati ya wafugaji na wakulima inasababishwa na vijiji vingi hapa nchini kuto kuwa na mipango ya matumizi bora ya ardh.
Akiongea mmoja wa maafisa ardhi wilayani mpwapwa Edina Nambua alisema kuwa kwa wilaya ya mpwapwa kuna vijiji tisa tu ambavyo tayari vimefanyiwa mpango wa matumizi bora ya ardhi kati ya vijiji 124.
Aidha Nambua alisema kuwa sababu nyingine inayao pelekea migogoro kati ya wafugaji na wakulima sehemu za vijijini ni baadhi ya watendaji wa ngazi za vijiji na kata kuwa sehemu za kusababisha migogoro hiyo kwa kushidwa kusimamai a sheria no 5 ya ardhi ya mwaka 1999ambayo hupelekea mianya ya rushwa,
Tena alisema kuwa mpango huo unagharama kubwa sana kitu kinachopelekea serikali kushidwa kuvifikia vijiji vyote juu kutengeneza mpango huo kwa vijiji vyote hapa nchini .
Alidai kuwa kati ya vijiji tisa vilivyo fanyiwa mpango wa mtumizi bora ya ardhi vjiji vitatu vya Pwaga ,Inzovu na Mingui vimefanywa na serkali kwa kupita mradi wa Mpango wa kurasimisha Rasilimali na biashara za wanyonge Tanzania (MKURABITA).
Na vijiji vingine vilivyo bakia ambavyo ni vijiji vya Lufusi Galigali Mbuga na kizi ni vijiji ambavyo vimfanyiwa mpango huo na shirika la kuhifadhi misitu ya asili TFCG lililoko wilayni mpwapwa katika kijiji cha mbuga.
Vjiji vingine vilivyo fanyiwa mpango huo ni vjiji vya Chunyu na Ngh`ambi ambavyo vimefanyiwa mpango na shirika lisilo la kiserkali la DONET la mkoani Dodoma .
Naye mratibu wa shirika la AFNET wilayani mpwapwa Bwana NOEL STEPHEN alisema kuwa katika hili serikali haina budi kulaumiwa moja kwa moja kwa kupanga mipango mingi lakini kushidwa kuitekeleza:mfano katika dira ya taifa ya ya maendeleo kipengele cha tatu kinacho dai kuimarika kwa uchumi imara na wenye ushindani kwa kuwa na vianzio mbalimbali vya uzalishaji na uchumi ambao unamaendeleo ya viwanda yaliyo karibu na nchi zenye mapato ya kati” alisema Stephen
Pia aldai kuwa serikali kama haikuweza kulifanya hilio mapema wakati tayari kuna viashiria vya watanzania wengi kuanza kuporwa ardhi zao na wageni kutoka nchi za jirani kwa kizingizio cha kuoa au kuolewa na muungano wa afrika mashariki.
Tena siku za karibuni kulizuka mgogoro wa wakulima na wafugaji katika kata ya masa amabapo baadhi ya watu kadhaa walijeruhiwa ambao ni wakulima na mifugo ya wafugaji ilijeruhiwa pia.
Comments
Post a Comment