mpwapwa waaswa kujiandaa na majanga ya mafuriko
Na noel Stephen mpwapwa
W ITO Umetolewa kwa wanachi wa wilaya ya mpwapwa kuweza kujikinga na majanaga ambayo yanaweza kuzuilika ili kuweza kupunguza matokeo ya maafa kwa jamii .
Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya mpwapwa BWANA Chrisopher Kangoye alipokuwa akifungua warsha juu kwa wakuu wa idara na wakuu wa tasisi juu kuweza kutumia rasilimali zilizopo kwa ajili ya kuweza kuzua majanga na mafuriko kwa wilaya ya mpwapwa.
Kangoye alisema kuwa kuna maafa ambayo yanaweza kuzuilika kama wananchi wanaishi mabondeni kuhama kabla maafa hayajafika na kuweza kuimarisha miundo mbinu kwa wilaya hiyo ikiwemo barabara, makazi, na madaraja.
AIDHA Kangoye alisema kuwa kwa historia wilaya ya mpwapwa inakabiliwa na majanaga kama mafuriko,uchomaji moto milima, kuanzia mwezi septemba hadi decemba ambapo alisema kuwa kutokana na hali hiyo wilaya na taifa inaingia hasara kubwa kwa kuwahudumia watu walio athiriwa na matukio hayo ambapo aliwataka wananchi kuchukua tahadhari mapema na kuacha tabia ya kusubili majanga ili wapate sababu za kuilaumu serikali.
Na alidai kuwa kwa wilaya ya mpwapwa inaingia hasara kubwa sana kwa kukosa usafiri, watu kufa na makazi yao kuharibiwa kwa mafuriko ya mvua ambayo hutokea vijiji vya msagali na gulwe kunzia miezi ya novemba na desemba ,hivyo aliwataka wananchi wa kata hizo na vijiji hivyo kuweza kuchukua tahadhari mapema kabla maafa hayajatokea.
Na alitoa kalipio kali kwa watendaji wa halimashauri hiyo ambao husubiri maafa kutumia fursa hiyo kuweza kujinufaisha wao kwa kujenga miundo mbinu chini ya viwango au kutumia fedha tofauti na malengo yaliyo pangwa.
KWA upande wake mkurugenzi wa kitengo cha majanga na maafa kutoka ofisi ya waziri mkuu Brigedia msatafu Dakson Mdoe alisema kuwa mpwapwa na kilosa ni miongoni mwa wilaya ambazo zinakubwasana na mafuriko kwa kipindi cha mvua za masika zinapo anza kunyesha katika wilaya hizo hivyo alitoa wito kwa uongozi wa wilaya na halmashauri kuweza kuzuia kuliko kupambana na matukio hayo kwa wilaya mabapo alisema gharama za kuzuia ni ndogo kuliko za kuweza kupamabana nayo majanga hayo.
Pia alisema imebainika kuwa wilaya hizo zinakubwa na majanga ya mala kwa mala kutokana na baadhi ya kata kuwa katika mkondo wa bonde la ufa ambalo huweza kusababisha matetemeko ya ardhi , na mafuriko.
Alieleza kuwa lengo la warsha hiyo ni wilaya kuweza kundaa mpango wa kukabiliana na maafa yanayoweza kutokea kwa kipindi cha miezi hiyo, na kuweza kuwashirikisha viongozi wa wilaya kuweza kubainisha fulsa zilizopo na vikwazo ili kuweza kupunguza matokeo ya maafa kwa kufuata sera ya taifa ya udhibiti wa maafa .
“ Kwa mfano mafuriko ya mwaka jana kukarabati miundo mbinu ya reli ya godegode na gulwe imigharimu serikali shilingi billion 5 ambazo ni fedha kubwa kwa nchi maskini kama Tanzania bora tungejipanaga tungeweza kufanya kitu cha maana naomba viongozi wote tushirikine katika hili ili kupunguza ukali wa maisha kwa mlipa kodi’’ alisisitiza MDOE
Wajumbe wa warsha hiyo waliweza kubainisha majanaga mabayo hui sumbua wilaya ya mpwapwa ambapo walisema kuwa ni magonjwa ya milipuko ya wanayama na binadamu,uchomaji moto misitu, mafuriko na matetemeko ya ardhi.
Comments
Post a Comment