LICHA ya Manispaa ya Dodoma kukusanya shilingi milioni 163,620,000 kwa mwaka katika kituo cha daladala cha Jamatin, bado kituo hicho kimejaa mashimo na takataka kiasi cha kuwa ni kero kwa wasafiri na kusababisha adha kubwa.
Waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo wamejionea uchafu na mashimo makubwa katika kituo hicho huku baadhi ya watu wakielndelea kulalamika kuwa wanapata kero kubwa.
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki wa daladala mkoani Dodoma(Uwedo), Ibrahimu Mohamed, amesema kituo hicho kina jumla ya daladala 889 na kati ya hizo 20, hiace.
Mwenyekiti huyo alisema gari hizo zinakusanya ushuru wa Sh 500 kwa daladala na hiace zinatozwa sh 100 kwa kila siku lakini hawajui fedha hizo zinepelekwa wapi.
Mohamed amesema kituo hicho ni kibovu na kinahitaji ukarabati mkubwa lakini tangu mwaka 2003 amekuwa akiufuata uongozi wa Manispaa kuhusu kufanya ukarabati lakini mpaka leo bado wanatoa majibu kuwa watatengeneza bila mafanikio.
Kiongozi huyo alisema alishauandikia barua uongozi wa Manispaa ya Dodoma na kufuatilia kwa zaidi ya miaka 8 lakini hakuna kinachoendelea zaidi ya kuambiwa kuwa watatengeneza tu.
Mmoja wa wasafiri katika eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Amina John, alisema kuwa kero wanayoipata katika kituo hicho ni kubwa na kwamba hawajui kama mahali pa kukimbilia.
“Hapa hatuna hata mahali pa kusimama kila mahali ni madimbwi na tope na katika madimbwi kuna vinyesi lakini katika kipindi cha jua tunaunguzwa kweli na jua,’’alisema John.
Alipotakiwa kuzungumzia kero hiyo,Afisa habari wa Manispaa ya Dodoma Gisela Mavela alisema kuwa kituo hicho kiko katika orodha ya maeneo yanayotakiwa kufanyiwa ukarabati.
Mavele alisema Manispaa ya Dodoma kwa kushirkiana na benki ya dunia wametenga fedha nyingi ambazo zitatumika kwa ajili ya kukarabati kituo hicho pamoja na stendi ya mkoa ya Dodoma.
“Siwezi kusema kwa sasa ni kiasi gani kimewekwa kwa sasa inabidi kwanza niwasiliane na wahusika ili nijue kiasi kamili kilichotengwa kwani siwezi kusema jambo lololote kabla ya kupata udhibitisho,’’alisema Mavele.
Alipotakiwa kuzungumzia fedha zinazokusanywa katika eneo hilo alishtuka na kusema “ ehe, kwani kweli tunakusanya kiasi hicho, mbona kasheshe hiyo, mimi sijui kama tunakusanya kiasi hicho lakini nitalifuatilia,’’alisema mavele
Mwisho.
GROUP NAMBA 3
ReplyDelete