BABA AMBAKA MWANAE WA MIAKA 12 NA KUMMPA MIMBA.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Jemsi Leuna mkazi wa kijiji cha Chitemo wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma amefikishwa mbele ya hakimu makazi mfawidhi bi Nurupedesia Nassar kufutia tuhuma ya kumbaka na kummpa mimba mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 12 mwanafunzi wa darasa nne. Mwendesha mashitaka wa polisi Bwana Michael Joseph aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo akitambua kuwa huyo ni mtoto wake wa kumzaa aliweza kumbaka na kutenda kosa hilo kinyume na kifungu cha namba 130 kifungu kidogo(1) na kifungu 131kifungu kidogo(1)iliyo fanyiwa malejeo mwaka 2002. Bwana Machael aliiambia mahakama kuwa kosa la pili ni kummpa mimba mwanafunzi darasa la nne kinyume na sheria ya Elimu namba 353 kifunfu cha 60Akifungu kidogo cha kwanza iliyofanyiwa malejeo mwaka 2016. Mtuhumiwa alipo ulizwa juu ya tuhuma hizo alikanusha kutenda kosa na kesi yake iliahirishwa...