UWIZI PUNDA UTAONGEZA UMASKINI VIJIJINI
.
Serikali imeobwa kuweka mkakati maluum wa
kudhibiti wimbi la uwizi wa punda ngozi ya Punda
kutokana na mnyama huyu kuwa
katika hatari kubwa ya kutoweka nchini
na hivyo kusabisha kuongezaka kwa wimbi la umaskini kwa jamii nyingi za
vijijini zinazo mtegemea mnyama huyu.
Matukio ya uwizi wa punda yamekuwa yakiongeeka kila kukicha sehemu
mbalimbali za wilaya ya Mpwapwa na mkoa
mzima wa Dodoma.
Katika Tukio lililotokea katika kijiji Mzase kata ya Berege
wilayani hapa punda watano wamekutwa wameibwa na kuchunwa ngozi huku mizoga yao
ikiwa ametelekezwa porini.
Mmoja wa wanakijiji hicho
bwana Naftari Asheri amesema kuwa endapo jitihada za makusudi
hazitachukuliwa za kuweza kuokoa uwizi
wa punda kuna uwezekano mkubwa wa wanyama hao kutoweka na na hivyo kusababisha ongezekao la umaskini
sehemu za vijijini kulingana na umuhimu wa mnyama huyo katika maisha ya
Mtanzania.
Aidha Bwana Naftari alisema kuwa lazima serikali iweke mkakati madhubuti wa kukabiliana na changamoto ya
kumuokoa mnyama huyo ambae siku za hivui karibuni amekuwa akiwindwa zaidi kuliko mnyama yeyote Yule.
Dkt. Kahema alisema kuwa kutokana na kuzidi kushamili kwa biashara hii ya ngozi
za punda katika jamii kunatishia wanyama
hawa kuzidi kupungua siku hadi siku na kusababisha kupungua kwa nguvu kazi ya mfugaji wa punda kila kukicha.
Aidha Dkt Kahema alisema kutokana na utafiti uliofanywa na shirika hilo imebaini kuwa kila siku punda zaidi ya mia moja wanauwawa kila siku kwa kuchinjwa kama kitoweo au kwa ajili ya kuuza ngozi yake katika
viwanda vya wachina vilivyoko Dodoma na Shinyanga na katika jamii.
Aidha
alisema kuwa kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa
ndani ya miaka mitatau mbeleni taifa litakuwa halina mnyama kazi kama punda kutokana na biasahara ya ngozi yake kushika kasi sana katika bara la asia hasa
nchini China.
Hata hivyo Dkt Kahema alisema kuwa kwa sasa Tanzania inakadiliwa kuwa na punda
wasio zidi laki tano nchi nzima lakini
uwiano wa uzalishaji na uchinjaji wa Punda kwa siku haviendani na kutishia
mnyama huyo kutoweka kabisa
katika jamii.
Alidai kuwa
Punda amekuwa akifanya kazi za kila siku za mwananchi wa hali ya chini
kijijini hivyo mnyama huyu akipotea basi wimbi la umaskini litaongezeka hapa
nchini.
“ Unajua kwa sasa punda mzima uanauzwa kwa
shilingi laki mbili wakati kwa mwaka
punda anafanya kazi za zaidi ya milioni tano kwa mkulima kama kulima,kuchota
maji, kubeba mizigo na shughuli zote
kila siku kwa mkulima”aliongea Dkt Kahema.
Alisema kutokana na ugumu wa maisha ya
mnyama huyu uzalishaji wake kwa mwaka umekuwa wa shida ambapo punda hubeba
mimba kwa miezi 12 na na huingia joto mala baada ya miaka mitatu hivyo
huzalishaji wake umekuwa ni mdogo sana ukilinganishwa na upoteaji wake katika
jamii.
Comments
Post a Comment