JESHI LA POLISI LATEKETEZA HEKALI 11 ZA BANGI MPWAPWA.
Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma imekamata na kuteketeza hekali
11 za bangi katika safu za milima
Galigali kitongoji cha Dibulilo.
Kamati hiyo iliyo ongozwa na mwenyekiti wa kamati ambae ni mkuu wa wilaya ya Mpwapwa bwana
Jabiri Shekimweri juu ya oparesheni ambayo ni mkakati wa kupambana na
madawa ya kulevya wilayani hapa.
Mkuu wa wialaya ya
ampwapwa bwana Shekimweri alisema kuwa
mkakati wa kutokomeza madawa ya
kulevya ni endelevu katiika wilaya yake na hivyo lengo kuu ni la kukisaidia kizazi cha wana
mpwapwa cha sasa na badae kwa
mstakabali wa taifa zima.
Aidha Shekimweri amewataka
watenadaji wa kata na viiji kuweza kuweka mkakati huo kwa nagazi ya kijiji,
kata na tarafa .
Alisema “Nina wataka watendaji wote wa kata na vijiji kuweza
kuweka mkakati huu wa kupambana na madawa ya kulevya kwa ngazi ya kata na
tarafa na yeyete kwenye kata yake ikabainika kuna ulimaji wa bangi na bila yeye kutoa taarifa atahusishwa
katika makosa hayo”aliongea Shekimweri.
Kwa upande wake Mkuu
wa polisi wilayani hapa bwana Edwin Mafuru amesema
waliokamatwa kwenye tukio hilo ni
mzee Felisian Mwamba na mototo wake
mwenye umri wa mika 14 mwanafunzi wa darasa la sita.
Bwana Mafuru alisema
kuwa kutokana na Jiografia ya
wilaya ya Mpwapwa kuzungukwa na milima kuna wa tu wengi wanaojihusisha na ulimaji wa Bangi katika safu za milima Galigali,Kibriani.Chogola
,Chinyika na Milima ya Mang’aliza .
Hata mrakibu wa polisi
huyo alisema “ haiwzekani
mtu analima bangi miaka mitatu
mfulilizo na anazidi kuongeza eneo
kila mwaka lakini taarifa hazitolewi
hivyo kunatupa shaka kuwa watu wengi wanahusika katika hili wakiwemo
viongozi wa vijiji na kata ninaomba iwe mwisho jeshi la polisi halijalala tutashughulika na kila atakae jihusisha katika vita hii” alifafanua bwana
Mafuru
Mmmoja wa wana
kijiji hicho bwana Jastini
Mnyalwao alisema kuwa kutokana na watu kupenda maendeleo ya haraka
haraka na njia za mkato hujiingiza katika biashara haramu za ulimaji uzaaji na
usambazaji wa bangi , kitu alicho kiseema kuwa kinaathiri taifa na kizazi cha
watanzania.
Uchunguzi uliofanya na Gazeti hli umebaini kuwa baadhi ya viongozi wa vijiji na kata
wamegeuza wakulima wa bangi kama kitega uchumi
kwa kupewa kitu kidogo ili wawafuchie siri zaulimaji wa bangi katika milima hiyo.
Comments
Post a Comment