UGONJWA WA NGURUWE WAWATIA UMASKINI WAFUGAJI MPWAPWA.
BAADHI yawafugaji
katika wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wameingia hasara kwa kupoteza mifugo yao aina ya nguruwe kutokana na kuzuka kwa
ugonjwa wa nguruwe ujulikano kama
African swine fever.
Wakiongea na Gazeti hili
kwa nyakati tofauti mmoja wa
wafugaji bi Tabitha Simbeye alisema
tangu ugonjwa huo uzuke wafugaji wengi
wamepteza nguruwe wengi na hivyo kuwasababishia hasara kubwa.
Tabitha alisema
katika mtaa wake zidi ya zizi lake kulikuwa na nguruwe sita wote
walikubwa na ugonjwa baadhi alifanikiwa kuwauza kwa hasara na wengine walikufa
na kuwazika.
Alisema nguruwe wengi yameathiliwa na ugonjwa huo
ambapo alisema Nguruwe hutetemeka na kukosa nguvu . kushidwa kutembea.
Aidha mmoja wa
watafiti wa mifugo kutoka katika
Tasisi ya utafiti wa mifugo TARILI
Mpwapwa ambae jina lake hakutaka liiandikwe alisema kuwa ugonjwa ambao
hutokea kwa msimu hiyo na ni ugonjwa unao sababishwa na virusi hivyo
ni ngumu kutibika wala kukinga.
Mtafiti huyo alisema ili kuweza kudhibiti ugonjwa huo ni
kupiga karantine za shughuli zote za mifugo ikiwemo minada na shughuli zingine zote ili kuzuia ugonjwa
huo kuenea kwa wingi.
Kwa upande wake
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mpwapwa bwana Mohamed Maje alikili kuwepo kwa ugonjwa, kuzuka
kwa ugonjwa huo wilayani kwake huo uliotekea mkoani morogoro na
alisema tayari alishatoa maelekezo kwa maofisa mifugo ngazi ya kata na vijiji
ikiwemo kusitisha shughuli zote zinazohusiana na uchinjaji,uuzaji na na
usafirishaji mazao yote yatokanayo na Nguruwe.
Aidha Maje
alisema ugonjwa huo unaenezwa na kirus
na husababazwa kwa hewa na hivyo kuna
hatari ya wafugaji wakapoteza nguruwe wote
ndani ya wilaya maaeneo ugonjwa uliko iingia. Kwa nature ya ugonjwa huu
hana dawa wala kinga na hivyo ukiingia
eneo Fulani hakuna njisi pia kuna
wasiwasi wafugaji wanaweza kupoteza nguruwe wote katika maeneo ugonjwa ulipo
ingia.
Hata hivyo Maje alisema kutokana na ugonjwa huo umeweza
kuadhiri uchumi wa mwananchi na halmshauri kwa kodi zilizo kuwa ninalipwa na
wafanya biashara wa mabucha ya nguruwe na ushuru wa majichio.
Pia aliwataka Wafugaji
kuweza kujiunga kwenye
vikundi ili kuweza kuwa na sauti ya
pamoja na katika kuzikabili
changamoto za mifugo ikiwemo
kinga kwa wanyama wao na matibabu pindi ugonjwa utokeapo.
Pia maje alitumia fursa hiyo
kuwataka wafugaji kuzika mizoga ya nguruwe wanao kufa au kuteketeza kwa
moto ili kuogopa ugonjwa huo kuendelea kuenea katika maeneo mengine ndani mkoa mzima.
Comments
Post a Comment