Imeelezwa kuwa
shughuli za ajira muda
zilizofanywa na walegwa wa mpango wa kaya maskini TASAF awamu ya tatu kama
kutunza Misitu ya asili,uvunaji wa maji ya mvua, na utunzaji wa udongo,ikitumika
inavyopaswa itaweza kuleta mabadiliko
chanya kwa jamii na kuweza kujiletea maendeleo endelevu.
Kauli hiyo imetolewa na
Mratibu wa Tassaf wa halmasahauri ya wilaya ya Mpwapwa Bwana Paskal Jeremia alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu
tadhimini ya utekelezaji wa mpango wa
ajira za muda zijulikanozo kama (PWP)kwa wanufaika wa mpango huo wilayani hapa
Jeremia amesema rasilimali hizo kama ujengaji wa miundo mbinu
ya kuvuna maji ya mvua, wa utunzaji wa misitu, na uhifadhi wa
udongo ngazi ya jamii italeta mabadiliko kuwa mazuri zaidi
na jamii kuweza kujiletea
maendelea endelevu katika maeneo yao yanayoishi.
Aidha amesema kwa sasa zoezi hilo limetekelezwa kwa
zaidi ya asilimia 70% katika vijiji vyote
ambavyo mradi huo ulitekelezwa
bali amesema kuna baadhi ya changamotozilizojitokeza kama za malipo ambazo
makao makuu yanazifanyia kazi na walegwa watalipwa muda si mrefu.
Amesema
Mpango wa Tassaf katika awamu
zote tatu umeweza kuonyesha mafanikio
mazuri ngazi ya jamii na halmashauri
kwa walegwa walioko kwenye mpango wameweza kubadilisha maisha yao kwa kujiibulia miradai
midogomidogo na kuweza kumubudu maisha yao ya kila siku.
Kwa upande wake ofisa
ushauri naufuatiliaji wa Tassaf wilayani hapa bwana Hosea Sichone amesema madhumuni ya
mpango ni kuziwezesha kaya
maskini sana kuongeza matumizi muhimu
kwa jia endelevu na kuziwezesha kaya
hizo kuwa na pesa za matumizi wakati
kipindi kigumu zaidi.
Hata hivyo Hosea amesema
kuwa pia madhumuni mengine ni kuwekeza katika rasilimali watu hasa watoto ikiwa na lengo la kuaandaa kizazi
chenye tija ,kuimarisha shughuli za
kuongeza kipato na kuongeza shughuliza za huduma za jamii.
Mmmoja wawanufaika wa
Mpango huo Bi Maligalitha Chinoga amesema kuwa
miradi ya kutoa ajira za muda kwa
kaya maskini japo kuwa unalenga
katika utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya hali hewa lakini lakini uharibifu
mkubwa wa mazingira katika wilaya yetu unatishia uendelevu wa miradi hiyo.
Comments
Post a Comment