WAGANGA NA MANESI WAONYWA KUTOA HUDUMA KIMAZOEA




SERIKALI  wilayani Mpwapwa moani Dodoma imewata wanganga na manesi wilayani hapa kuweza ku kufanya kazi yao kwa kufauta maadili ya kazi ili kuweza kuokoa maisha ya wagonjwa .
Kauli hiyo ilitolewa na mwenyekiti ya kamati ya ulinzi na usalama na  mkuu wa wilaya hiyo  bwana  Jabir Shekimweri  alipopanya ziara za kushitukiza katika  vituo  vya afya na zahati  za serikali na za umma  kwa lengo ya kujionea huduma zinazo tolewa na vituo hivyo na  miundo mbinu yake.
Shekimweri alisema kuwa  ameamua kufanya ziara hiyo ili kuweza kuona huduma za afya zinavyo tolewa na vituo hivyo  na  changamoto zinazo vikabili vituo hivyo na njisi ya kuondokana nazo.
Aidha  shakimweri alisema  serikali ikiwa inajiandaa kuhamia  mkoani Dodoma lazima wilaya za mkoa huo kujipanga kuboresha huduma za jamii   ikiwamo afya ambayo ndio msingi mkuu wa  huduma zote  katika kuwekeza katika taifa lenye rasimali watu na wazalishaji .
Hata hivyo  Shamweri alisema kuwa pamoja na ziara hiyo ameabaini baadhi ya mapungufu  katika vituo na vya afya na  zahati  za mjini hapa ikiwa ni  upungufu wa watumishi katika utunzaji mbovu wa dawa katika stoo zao na baadhi ya dawa  zinazokaribia matumizi yake kuisha na zinngine zikiwa zimeisha matumizi yake .
Pia shemweri  alikri wilaya yake kukabiliwa na   uhaba wa watumishi  wa watumishi wa afya kunakopelekea malalamiko ya watu na baadhi ya maeneo kukosa huduma  au kupata huduma chini  kiwango kilichotarajiwa.
Hata hivyo Shekimweri  alitumia fursa hiyo kuiomba  serikali alisema ujio wa wa serikali  mkoani Dodoma uataweza  kufungua  milango ya wageni wengi na idadi ya watu kuongeza kwa wingi ndani ya wilaya  yake  hivyo lazima ajipange mapema.
“Tunajua seriakli  inahamia mkoani   Dodoma  hivyo lazima tujipange kupokea huo ugeni na huduma tulizo nazo hasa huduma za afya kwa maana kwa sasa  wilaya yangu  ina watu  32,4681 hivyo lazima tuone uwezekano wa kuwa na huduma bora na kuboresha miundo mindu yetu lankini wafanya kazi kuweza kuacha kufanya kazi kwa mazoezi.”aliongea Shekimweri.
Kwa upande mganga mkuu wa wilya Dkt Said Mawji alisema  wilaya inavituo 55 vya kutolea huduma za afya zikiwamo vituo vya afya pamoja na zahati lakini alikili vituo hivyo kukabiliwa  na upungufu wa  watumishi  ambao unatishia  huduma kutolewa chini ya kiwango.
Mawji alisema kwa mujibu wa sera ya afya zahati zinatakiwa kuwa na watumishi 15, kituo cha afya watumishi 39, wakati hospitali inatakiwa kuwa na watumishi  200 wakati vituo vingi  ikama haitoshi kutokana na uhaba wa watumishi wa afya hapa nchini.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.