KIPINDIPINDU CHAUWA WAWILI MPWAPWA.
JUMLA
ya watu 94 katika
wilaya ya Mpwapwa katika mkoa wa Dodoma wamegundulika kuumwa ugonjwa wa kipindupindu wakati wawili tayari
wamesha fariki Dunia kutokana na ugonjwa huo.
Hali
hiyo imeelezwa mganga mkuu wa ya wilaya ya Mpwapwa Dkt Siad Mawji alipokuwa akiongea na waaandishi wa habari juu ya kuwapo kwa wa ugonjwa huo
katika wilaya hiyo na kusabaisha hali ya
wasiwasi kwa wakazi wengi wa wilaya hiyo na viunga vyake.
Dkt
Mawji alisema kuwa mgonjwa wa
kwanza aligundulika octoba
26 mwaka huu akitokea kata ya Mweznele na wagonjwa wengene waliendelea kujitokeza
kutoka katika kata mbalimbali hadi kufikia wagonjwa 94 tangu ugonjwa huo uanze hadi sasa.
Hata
hivyo alisema w wagonjwa wengine walitokea
katika kata ya Tambi,Mpwapwa mjini,
Lumuma na Matomondo na kufanya wagonjwa
wote kufikia wagonjwa 94.
Aliongeza
kuwa hada kufikia jana ni wagonjwa kumi
na watano 15 ndio waliolio lazwa katika kambi maluum ya kuwashughulikia wagonjwa
wa kipindupindu na wagojwa 71 tayari
hali zao zimekuwa nzuri kurudi tena
majumbani mwao wakati wagonjwa wawili walifariki dunia.
Aidha
alisema chanzo kikubwa cha ugonjwa huo
katika kata hizo ni kutokana na kuwapo kwa tataizo la uhaba wa maji na hivyo watu hulazimika kutumia maji ambayo
si safi na salama ambayo ni maji ya
mtiririko baada ya visima vyao kuharibika .
“Katika
katazenye ugonjwa wa kipindupindu tatizo kubwa la maji safi na salama kutokana na
hali hiyo watu wanatumia maji amabayo si safi na salama ambayo ni maji ya visima vifupi na maji ya mtiririko ambayo si salama
sana”aliongea aiongea Dkt Mawji
Alisema
chanzo kingine kilicho changia kuenea
kwa ugonjwa huo kirahisi ni watu
wengi katika kata hizo kuto kufuata
kanuni za afya na kuto kuwa na vyoo pia mwingiliano wa watu katika kata za
mipakani kama kiosa na Gairo,kusababisha
ugonjwa huo kulipuka kutokana na husaidi kusambaza wadudu hao kirahisi
na maji machafu kunchanganyika na maji
ya visima.
Alisema kutokana
hali hiyo wamechukua hatua ya
kutibu maji yote ya visima kwa
kuyawekea dawa maluum ilikuweza kuweza kuua wadudu wote ambao wanaweza kusambaza ugonjwa huo kwa watu kirahisi na
kuwahamasisha watu kufuata kanuni za afya.
Dkt
Mawji alisema kwa sasa wananchi
wanapatiwa elimu ya kuhakikisha wanaishi
katika mazingira salama
ikiwa ni pamoja na kuwa
na vyoo bora kwa lengo la kujiepusha na mlipiko wa
magonjwa kama hayo na magonjwa
mengine ya mlipuko.
Mbali
na hilo alisema katika kata ambazo
wagonjwa wametoka kwa wingi wametakiwa kuunda kamati za kudhibiti na kutoa elimu ya kanuni za afya na sula la usafi wa mazingira ili watu na jamii hiyo kuishi katika mazingira mabayo ni salama zaidi.
Katika wilaya hii tayari watu wawili kutoka katika
kata ya Mwezele,na Lumuma wamesha poteza maisha
kautokana na ugonjwa huo.
Kwa
sasa katika mkoa Dodoma wilaya ya Mpwapwa ni miongoni mwa wilaya ambayo ugonjwa wa kipindupindu
umeumkumba kwa kasi ukiachilia mbali
wilaya ya kilosa na Gairo mkani Morogoro .
Mwisho.
Comments
Post a Comment