MPWAPWA YAMLIZA KAPONDA KIELIMU
OFISA elimu mkoa wa Dodoma Bwana Juma Kaponda (JJ)amewataka wataalamu ,wanasiasa, na walimu kushirikiana katika kushughulikia changamoto za Elimu ili kuweza kuinua elimu wilayani hapa. Kaponda aliyasema hayo wilayani hapa katika mkutano wa wadau wa elimu uliojumuisha , walimu wakuu wa shule zote, waratibuelimu kata , na na maofisa wa elimu , uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha ualimu Mpwapwa juu ya kutadhimini matokeo ya darasa la saba ya mwaka 2015. Kaponda alisema katika mtihani wa kumaliza elimu mwaka 2015 wilaya ya mpwapwa ilikuwa wilaya ya mwisho kimkoa na ilikuwa wilaya ya 164 kati wilaya 166 nchi zima ,japo ilifanikiwa kutoa mwanafunzi wa kwanza kimkoa kutoka katika shule ya Mazoezi Mteajeta mwanafunzi Airene Chiwanga Aidha alisema ufundishaji mbovu,utendaji wa kimazoea ...