WANASISA NA WATUMISHI WAASWA KUSHIRKIANA KUILETEA JAMII MAENDELEO ENDELEVU.
Na noel Stephen mpwapwa.
WATENDAJI na wanasiasa
wilayani mpwapwa wanatakiwa kushirikiana
katika kuiletea wilaya hiyo maendeleo endelevu.
LAI hiyo imetolewa na katibu Tawala wa wilaya hiyo Athanasia Kabuyanja alipokuwa akiongea na waaandishi wa habari
ofisi kwake mapema wiki kwa mahojianao maluumu.
Kabuyanja
aliwataka watumishi na watendaji wa serikali kuweza kushirikiana
katika kuiletea wilaya hiyo
maendeleo endelevu juu juu
kilimo, utunzaji mazingira, utawala bora na huduma za jamii ili mtanzania aifurahie
nchi yake na anufaike na kodi anazo lipa.
ALISEMA kwa wilaya ya mpwapwa ni miongoni mwa wilaya amabazo
ziliweza kuingia katika migogoro ya kiutendaji kati wa
watumishi na wanasiasa kwa mwaka 2013
kitu alicho kisema kuwa kwa sasa hali
hiyo imetulia na ushirikiano umemalika.
Aidha alisema “kunapokuwa na migogoro katika halmashauri yoyote ile kuna kuwa
hakuna ufanisi wa kazi hivyo watu
wanabaki kutatatua migogoro tu kuliko kufanya kazi za maendeleo za
kuwaletea wanachi maendeleo”aliongea na
kuongeza kabuyanja.
Pia aliwataka
watendaji wote wa kata na vijiji
kuzingatia utawala bora na misingi yake ili kuweza kuondoa kasumba ya
baadhi ya watendaji wa kata na vijiji kuwa ni miongoni mwa viongozi
wanao kiuka misingi ya utawala bora kwa kuendeleza hongo na rushwa.
ALIWATAKA wanachi wa
wilaya ya mpwapwa kuweza kutoa
taarifa za ukiukwaji wa misingi
ya utawala bora pale ambapo
wanapoobwa rushwa au hongo yoyote ili kuweza kupata haki ya kuhudumiwa kitu alicho kisema kuwa
kupata haki ni haki ya kila
mtanzania pasipo kujali kipato, njisi ,
kabila wala ukoo wote wanahaki sawa mbele ya jamii na sheria.
Comments
Post a Comment