UHABA WA MAJI MPWAPWA
Na noel Stephen
–mpwapwa
Kuna uwezekano mkubwa
wa kuzuka kwa magonjwa milipuka
kama kipundupindu na magonjwa ya kuambukizwa katika tasisi nyingi
zikiwemo vyuo, shule za sekondari
na maeneo ya mikusanyiko ya watu wilayani mpwapwa mkoani Dodoma kutokana
na kukosa huduma yamaji kwa siku tatu
mfululizo sasa.
AKIONGEA na mwandishi
wetu wilayani hapo kaimu mkuu wa shule
ya sekondari ya mpwapwa Sisti Karia alisema kuwa katika shule yake kumekuwako na
hali mbaya kiafya hasa maeneo ya
vyooni kutokana na kukkosekana kwa
maji katika shule hiyo.
Alisema kwa sasa shule
hiyo imeamua kuendesha shule kwa maji ya
kununua katika matoroli ambapo kwa dumu
wananunua sh 500/=hadi 1500/=kwa dumu la lita ishirini ambapo alisema
napo hali hiyo haitoshelezi
mahitaji ya shule kwa wanafunzi
kuoshea vyombo,kuoga na kuendea vyooni”kwa sasa tuna hali mbaya sana hasa
vyooni maana maji haya yanatosheleza
kupikia chakula tu hata maji ya kunywa yanakosekana sasa hali ikiendelea hivyo si tutauwa watoto
wa watu hapa endapo magojwa ya mlipuko
yakitokea au homa ya matumbo
tutafanyaje?aliongea Karia na
kuongeza.
AIDHA mwandishi wetu
alipo zungukia katika tasisi nyingi wilayani hapo alibaini hali bado mbaya hasa katika chuo cha ualimu Mpwapwa, chuo cha mifugo Visele
na sehemu za migahawani.
Kufutia hali hiyo
wilaya hiyo kwa imekosa huduma
ya nyama kutokana na wachinjaji kuto kuchinja kwa sababu ya kukosa maji ya
kuoshea nyama hizo ambapo watu wengi
hasa wafanya biashara ya nyama wameingia hasara kutokana na hali hiyo.
Kwa upande wake meneja wa
mamalaka ya maji safi na maji taka
MPWAUSA SHADRECK MATEMBA amesema
tatizo hilo limetokana na kuungua kwa
Transifoma ya umeme karibu na
kisima chao cha maji kilichopo vianze kikombo.
Pia ameongeza kuwa
kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha wilayani hapo miundo mbinu
mingi ya maji imeng’olewa na mvua hivyo kusababisha maji kuto ingia
katika matenki yake,
Na alisema kutoka na kuanguka kwa nguzo tisa za umeme eneo la chalinze nalo limechangia maji kuto kurudi kwa muda ulio kusudiwa wilayani hapo.
Matemba amewataka wanachi kuwa wavumilivu wakati mamlaka ya maji wilayani mpwapwa wakishirikiana na shirika la
umeme TANESCO wakijaribu kulitatua tatizo hilo
na kurudisha katika hali yake ya
kawaida.
Wadau wa maji mjini
hapa wameishauri mamlaka hiyo kuto kuwa na chanzo kimoja cha maji bali wajaraibu kuwa na vyanzo vingi iwezekanavyo ili kuweza kuokoa maisha ya watanzania kwa kuwa na mtanteki makubwa ya kuvuna maji
mvua ili kuweza kuyatumia pindi inapo tokea dharura kama hii ya kukatika kwa
maji siku tatu mfululizo.
Comments
Post a Comment