CHAMA CHA WALIMU CHAIDAI SERIKALI MILION 412.7 MPWAPWA
Na noel Stephen - Mpwapwa
CHAMA cha walimu wilayani mpwapwa mkoani Dodoma
kinaidai serikali kiasi cha tsh milioni 412,701,983 kama madeni ya mapunjo ya mishara,
pesa za likizo na upandishwaji wa madaraja. Kwa walimu wake kwa kipindi cha kuanzia desemba 2012 na hadi
feb 2014.
Kauli hiyo imelotelewa
na katibu wa chama hicho wilayani hapa Donard
Kisamaba alipokuwa akisoma taarifa ya
utekelezaji katika mkutano mkuu wa mwaka
wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa ccm mjini mpwapwa.
Kisamba alisema
kuwa madeni hayo ni mapunjo ya mishahara
na makato mbalimbali ambayo walimu
wanamdai mwajili kama haki zao za msingi
kazini .
ALISEMA serikali ikiwa
katika mchakato wa matokeo makubwasasa
(big result now) katika idara ya elimu hayatapatikana kama serikali
itaendelea kuviona vyama vya wafanya kazi kama ni adui wa serikali au wachochezi wa migogoro mahali pa kazi kitu alicho kisema kuwa ni mtazamo hasi wa
serikali kwa vyama hivyo.
AIDHA alisema kuwa
vyama vya wafanyakazi sio adui wa
serikali bali vipo kwa ajili ya
kuisaidia serikali kuweza kutoa
haki zinazo stahili kwa mtumishi ili mtumishi awe n maisha bora na aifurahie
kazi yake.
ALIDAI ili kuweza
kupima matokeo makubwa sasa serikali iweze kulipa madeni inayo daiwa kutoka
kwa wafanya kazi “ bila hivyo matokeo makubwa yatabaki katika mipango na
kwenye makaratasi lakini hayataonekana kwa jamii”alisema na kuongeza Kisamaba.
Katika mkutano huo
uliombana na uchuguzi wa viongozi
mbalimbali wa kukiongoza chama hicho ambapo John Kipalamoto alibuka mwenyekitiki mpya wa chama hicho kwa
kumshinda mpinzani wake Edward
Mwamakula kwa kura 32 kwa 29,
Nafasi ya mwakilishi wa
sekondari walibuka OMARY JUMA NA
AISHA Hamisi wakati nafasi ya mwakilishi
shule ya msingi alichaguliwa Savera Lasoya na
John kipalamoto alichaguliwa mwakilishi vyuo vya ualimu nafasi aliyo jitoa baada ya kushinda
nafasi ya umwenyekiti wa chama hicho.
Comments
Post a Comment