WAHUKIMIWA KWENDA JELA MIAKA MITATU BAADA KWA KUHARIBU MALI



Na noel stephen mpwapwa.

Hakimu mkazi Adrikian Kilimi wa Mahakama ya wilaya  mpwapwa imewahukumu kwenda jela miaka mitatu  bwana Patric Mwidowe,Sehewa Chitema, na Kedmon Chitema wakazi wa kijiji cha kiboroani  wilayani mpwapwa mkoani Dodoma  kwa makosa ya   kuvamia na kuharibu mali  na kuchoma mali za Tasisi  ya utafiti wa mifugo TALIRI .

Akieliza mbele mbele ya mahakama  hayo wakili wa serikali  Godfrey Wamabali alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa  walilifanya kosa hilo December 19,mwaka huu  katika maeneo ya kijiji cha kiboriani wilayani mpwapwa mkoani Dodoma  wakiwa wote kwa pamoja,

Kesi hiyo iliyokuwa ikiwa kabili wakazi wa Kijiji cha Kiboriani   kata ya mpwapwamjini wilayani mpwapwa mkoani Dodoma  iiliyowahusisha   wanakijiji wa kijiji hicho hatimae ilifikia  kikomo chake  baada ya  mahakama kuwahukumu washtakiwa kwenda jela miaka mitatu  kwa makosa  ya  kuvamia na kuharaibu mali  na kuchoma moto mali za tasisi hiyo.

  Kwa upande wake  wakili  uapande wa walalamikiwa bwana Lussa David alidai kuwa  tasisi hiyo haikuweza kuzileta mali zilizo haribiwa  pale mahakamani  ili ziweze kuonwa na walalamikiwa na kiasi cha  uharibifu ulio tokea ,

Pia aliomba mahakama hiyo kabla hajatoa hukumu iliweza kwateteawalalamikiwa kuwa  washitakiwa wote wanawazazi wao wazee, wanafamilia zinawategemea  wakiwamo wake na watoto hivyo mahakama iweze njisi  kuwapuzia adhabu.

AIDHA hakimu mkazi  wa mahakama hiyo a Adrikian Kilimi  aliieleza mahakama kuwa  amzingatia maelezo ya upande wa utetezi na  pia ameweza kuangalia tasisi hasara iliyo ipata kutokana  na vitendo hivyo,

Pai aliweza kutoa maoni  kuwa  kumekuwakuwako na ongozeko la la vitendo vya wanachi wenye hasira kali kujichukulia  sheria mkoni vikiongezeka siku hadi siku  lakini mahakama haiwezi kufumba macho katika hili kwa maana mali zinazo haribiwa ni mali za walipa kodo wa Tanzania
.
Hivyo aliitaka jamii kufuata taraibu za  kisheria katika kutatua matatizo yanayo tokea katika jamii  kuliko kujichukulia sheria mkononi.

Akitoa  hukumu hiyo  alisema “ kosa la kwanza niwahukumu kulipa faini tsh 50.000/= elfu hamsini  kila mmoja  au kifungo mwaka mmoja jela  na kosa la pili la kuvamia mali   ninawahukumu kwenda jela miaka miwili kosa la tatu la kuchoma  niwahukumu kwenda jela miaka  mitatu , nitoa amri adhabu zote ziende sambamba”



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA YA MPWAPWA HATARINI KUTOWEKA

MAANA YA JINA MPWAPWA

DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.