MWENYEKITI AVULIWA MADARAKA KWA TUHUMA ZA KUCHAKACHUA PESA YA KIJIJI MRADI WA MAJI.
Na
noel stephen - Chipogolo mpwapwa
Wakazi
wa kijiji cha chipogolo wilayani mpwapwa
mkoani Dodoma wamemvua madaraka mwenyekiti wao wa kijiji Wilson Manemo kwa
tuhuhuma kununua Mashine mbovu ya kuvuta maji kijijini
hapo.
.
Waamuzi
huo ulichukuliwa na wanakijiji hao
kufutia mwenye kiti huo kukiuka
makabariano ya wanakijiji juu
ununuzi wa mashine ya desel ya kuvuta maji
kijijini hapo ambapo pamoja na wajumbe wengine wawili walinunua mashine
mbovu ambayo haifanyi kazi kwa gharama
tsh 8.500,000/=milioni nane na laki tano fedha za kijiji cha chipogolo.
Akiongea
na mwanachi kaimu mtendaji wa kijiji hicho
Yona Mganga alikili wananchi hao
kuvua madaraka c mwenyekiti wa kijiji hicho kwa madi ya kutumia vibaya fedha za
kijiji chao.
Mganga
alisema kufuatia mkutano wa kijiji ulio
kaa 17 april mwaka huu waliamua “kutokana
na uhaba wa maji uliopo katika kjijiji
hicho na kuharibika mashine ya awali kijiji kiliagiza fedha
zilizoko benki ya kjijiji zitolewe na
zika nunue enjinin mpya ili kuweza
kupunguza kero ya maji kijijini hapo”.
AIDHA
alidai kuwa “lakini kilichotokea mkutano
huo uliamua wajumbe wawili akiwemo
mwenyekiti wakanunue mashine nyingine mpya ya kuvuta maji kwa gharama y ashilingi million 6,500.000/=
matokeo yake wajumbe hao walileta
mashine ambayo imetumika na yenye
gharama ya tsh 8,500,000/= na
haivifanyikazi kabisa ni mbovu”alieleza mganga na kuongezea
Alidai
kuwa alipo fika wakati wa makabithiano
wajumbe wa kamati ya kjiji waligoma kupokea mashine hiyo kwa madai ya kuwa mashine hiyo ni mbovu na kuwataka
wajumbe walioenda kuinunua kuitolea
maelezo lakini walishudwa kuitolea maelezo ndipo wanakijiji waliikataa
kuipokea mashine hiyo
,
Mwandisi
wa maji wilaya ya mpwapwa Omar Mazola alikiri kuwepo kwa tatitizo hilo katika kijijiji cha chipogoro na aliahidi kulifanyia
kazi tatizo hili ikiwemo kuchukua hatua za kisheria kwa wote walio husika kwa
njia moja au nyingine pindi itakapo bainika kuwa mashine hiyo imechakachuliwa.
Alisema
kuwa mashine iliyo nunuliwa ni TR1 Desel
Engine ambapo amwewasilana na watu
wa TAMESA kuja kudhibitisha mashine hiyo kuwa ni mpya
au imetumika ili kuweza kuondoa utata
huo.
Mpaka sasa kijiji hicho bado kina kabiliwa na
adha kubwa ya ukosefu wa maji kutokana
na pamp ile iliyo kuwepo kharibaka hivyo
wananchi wa kijiji hicho hutumia maji ya kwenye madibwi amabayo si salama kwa
afya za binadamu.
Comments
Post a Comment