KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.
Mpwapwa. Habari. Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi Sophia Kizigo akiongea kwenye mkutano kazi wa RUWASA na wadau wa maji uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Afya.(picha na Emanuel Uronu(Vaino) Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma Bi Sophia Kizigo amezitaka jumuiya za watumia maji kuweza kuunganisha nguvu za jumuiya moja na nyingine ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi. Kizigo ametoa Rai hiyo wakati wa kikao kazi cha wadau wa maji kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha Afya mjini hapa kilicho wajumuisha Viongozi wa jumuiya za watumia maji watendaji wa kata na vijiji napamoja na madiwani wa kata husika , Kizigo amesema pamoja na serikali ya awamu ya sita kuweka dhamira thabiti ya kumtua mama ndoo kichwani lakini bado jamii husika imeendelea na uharibifu wa mazingira unaotishia uendelevu wa miradi mikubwa ya maji inayowekezwa na serikali. Kupitia changamoto hiyo...