KIZIGO AWAPONGEZA RUWASA,AKERWA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA,AWATAJA MADIWANI.
Mpwapwa. Habari.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi Sophia Kizigo akiongea kwenye mkutano kazi wa RUWASA na wadau wa maji uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Afya.(picha na Emanuel Uronu(Vaino)
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa mkoa wa Dodoma Bi Sophia Kizigo amezitaka jumuiya za watumia maji kuweza kuunganisha nguvu za jumuiya moja na nyingine ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kizigo ametoa Rai hiyo wakati wa kikao kazi cha wadau wa maji kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha Afya mjini hapa kilicho wajumuisha Viongozi wa jumuiya za watumia maji watendaji wa kata na vijiji napamoja na madiwani wa kata husika ,
Kizigo amesema pamoja na serikali ya awamu ya sita kuweka dhamira thabiti ya kumtua mama ndoo kichwani lakini bado jamii husika imeendelea na uharibifu wa mazingira unaotishia uendelevu wa miradi mikubwa ya maji inayowekezwa na serikali.
Kupitia changamoto hiyo ametoa siku 14 kwa madiwani wote wanasiasa na baadhi ya watendaji wa kata na vijiji wanaowakingia vifua waharibifu wa mazingira kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wote.
Aidha amedai jumuiya za watumia maji kuweza kufuata miongozo,kanuni na taratibu za utunzaji wa fedha zitokanazo na miradi ya maji katika vijiji, na kata ili kuweza kupunguza migogoro ya matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maji ‘’nina taarifa nyingi juu uendeshaji mbovu wa jumuiya hizi sasa kwa vile mmejengeana uwezo naamini mtaenda kubadilika wale ambao hawatabadilika tutajua za kufanya” aliongea
Hata hivyo Mhandisi Warioba alisema mpango wa kuunganisha jumuiya za watumia maji utaweza kuongeza ufanisi na kupanuka kwa huduma Zaidi lakini itapunguza gharama za uendeshaji na kuifanya miradi mingi kuwa na tija .
Amedai kwamba kwa sasa wilaya yaMpwapwa imeingia kwa Mpango wa lipa kutokana na matokeo hivyo lazima jumuiya hizo kuzingatia taratibu na sheria za uendelevu wa miradi.
Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Mpwapwa Cyprian Warioba akiongea kitu na wadau wa Maji katika kikao kazi kilichofanyikakatikaukumbi wa Chuo cha Afya.
Mhandisi Warioba alisema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali kupitia wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa)Mpwapwa imepanga kutekeleza miradi ya maji 15 katika maeneo mbalimbali itakayogarimu jumla ya shilingi 2,681,190,153.00 “na idadi ya watu wanaopata Huduma ya Maji Safi na Salama mpaka sasa ni watu wapatao 248,727 ambapo Sawa na asilimia 65.05.makadirio ya watu wapatao 320,891”
Mwenyeiti wa jumuiyaya watumia maji kautoka kata ya Chipogoro bwana Msafiri Mgonela (Punda wa Yesu) alisema katika kijiji chao wakati anaingia madarakani alikuta kijiji kizima kina vituo vine vya kuchotea maji na watu waliokuwa wameunganishiwa maji majumbani walikuwa watano “mpaka sasa watu waliunganishiwa maji majumbani ni themanini na watano kutoka kwenye watano,na kuongeza vioski vya kuchotea maji kutoka vitano hadi kumi na viwili lakini tasisi zote tumeshaziunganishia maji.
mwisho.
Comments
Post a Comment