DC KIZIGO ATOA MAAGIZO KWA KWA MAAFISA ELIMU KUKABILIANA NA UKATILI MASHULENI.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi Sophia Kizigo akifungua kikao cha wadau wa Ulinzi dhidi ya Mtoto na ukatili wa kijinsia kilicho wezeshwa na Jukwaa la utu wa Mtoto CDF wilayani Mpwapwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la utu wa Mtoto CDF Koshuma Mtengeti akichangia jambo katika kikao cha kujadili ulinzi wa Mtoto wilayani Mpwapwa.
Stephen Noel-Mpwapwa.
Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma Bi Sophia Mfaume Kizigo ametoa amri kwa maafisa Elimu wote ndani ya wilaya hiyo kuhakikisha shule zote za Msingi na sekondari zinakuwa na walimu walezi kwa lengo la kupunguza vitendo vya ukatili kwa watoto wawapo shuleni.Mkuu wa wilaya hiyo ametoa agizo hilo kwenye mkutano wa Siku moja uliondaliwa na Asasi ya kiraia jukwaa la utu wa mtoto CDF iliyo kutanisha Wadau wote wanao fanya afua za kumlinda mtoto na kujali ustawi wa mtoto.Amesema Ili kuhakikisha watoto wanakuwa Kwenye mazingira ya usalama lazima kunakuwapo na watu wanao ratibu kero zinazo wakabili watoto au pindi wafanyiwapo ukatili nyumban au eneo la Shule.
Bi Mary Jackoson Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake wilaya ya Mpwapwa akichangia jambo katika kikao cha Jukwaa la utu mtoto kilichofanyika katika umbi wa ofisi ya Mkuu wa wilaya May 17.2023.
"Sasa naagiza kwa maafisa Elimu wote Msingi na sekondari kuwa ifikapo kesho shule zote ziwe na matron na Patron hili halihitaji mpango kazi lifanyiwe kazi mala moja"Alieleza Kizigo.Kaimu Ofisa Elimu sekondari bwana Ally Akida amesema Kwa Sasa Mpwapwa ina Shule 33 za sekondari ambazo jumla ya wanafunzi 17,249 na wanafunzi waliopanga vyumba (mageto) ni wanafunzi 1204 ambao hujilea wenyewe na wapo Katika hatari kubwa ya kufanyiwa ukatili kutokana na mazingira wanayo ishi.Afisa Elimu Msingi Bwana Jackson Mpankuli amesema kuhakikisha watoto wanakuwa Katika usalama wa ni wajibu wa wazazi,/ walezi na walimu wanashirikiana Katika malezi ya watoto wao.Ofisa wa dawati WP 2420 Sanjeti Magreth amesema kuanzia mwezi March jumla makosa 15 ya ubakaji yalilipotiwa katika kituo cha polisi , makosa matano ya ulawiti yalilipotiwa na makosa mawili ya kuwapa wanafunzi mimba yalilipotiwa kuanzia mwezi March 2023.
Kwa upande Wake mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la utu wa mtoto Koshuma Mtengeti alisema tangu shirika hili lianze kufanya kazi katika wilaya hiyo mwaka 2017 wamefanikiwa kupunguza vitendo vya ukatili wa Kijinsia kwa Jamii ikiwemo kwa watoto wa kike,pia amesema wameongeza uelewa kwa jamii ambapo umesababisha taarifa za vitendo vya ukatili kulipotiwa Katika vyombo vya kutoa maamuzi.
Mwisho.
Comments
Post a Comment